Translate this blog in your favourable language

My pager view

Friday, January 7, 2011

JE USAWA WA KIJINSIA NI HALALI HATA KAMA DINI HAZITAMKI SANA HILO/

ipo hatari ya wanaume kuwa chambo sasa be care men
by STEVEN..
Usawa wa kijinsia ni lengo la kuleta usawa katika ya jinsia zote, kutokana na imani(belief) kuwa kuna udhalimu mbalimbali wa jinsia moja.
wapigania haki
Mashirika ya Dunia yamefafanua usawa wa kijinsia ikihusiana na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na maendeleo ya kiuchumi. UNICEF inafafanua usawa wa kijinsia kama "kusawazisha uwanja wa kucheza kwa wasichana na wanawake kwa kuhakikisha kwamba watoto wote wana fursa sawa ya kuendeleza vipaji vyao.
Idadi ya Watu ya Umoja wa Mataifa(United Nations Population Fund) ilitangaza usawa wa kijinsia "kwanza kabisa kama haki ya binadamu." Usawa wa kijinsia" ni mojawapo wa malengo ya mradi wa Milenia wa Umoja wa Mataifa , wa kumaliza umaskini ulimwenguni ifikapo mwaka wa 2015; mradi huu unadai, "Kila Lengo lina uhusiano wa moja kwa moja na haki za wanawake na jamii ambazo wanawake hawana haki sawa kama wanaume kamwe haziwezi kufanikisha maendeleo katika namna endelevu.
Hivyo basi, kukuza usawa wa kijinsia kunaonekana kama himizo kwa mafanikio makubwa ya kiuchumi. Kwa mfano, mataifa ya Kiarabu ambayo yanawanyima wanawake usawa wa kijinsia yalionywa katika ripoti iliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mwaka wa 2008 kwamba kitendo hiki cha kuwanyima mamlaka wanawake ni kipengele muhimu kinachodhalilisha kurudi kwa mataifa haya katika nafasi ya kwanza ya viongozi wa dunia katika biashara, elimu na utamadunI..
utata wa semenya nao unaashiria nini?
LAKINI KUNA KITU LAZIMA TUKAE TUKIJUA YA KUWA MAANDIKO MATAKATIFU HAYATAMKI HIVYO NA KUMPA USAWA MWANAMKE AWE SAWIA HATA KIMAAMUZI KIUONGOZI NA KIMADARAKA NI HATUA YA KUPINGANA NA MAANDIKO YA MUNGU KWANI KIOLA MMOJA KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE WALIWEKEWA MIPAKA YAO NA HATA SASA MFUMO ULIOPO DUNIA IMESHIKWA NA WANUME SASA TUNAPOTAKA USAWA ITAFIKA KIPINDI SASA WANAWAKE WATATAKA WANUME NA SISI TUFANYIWE MPANGON TUBEBE MIMBA SAWA KWA SAW A
   SIKATAI TUSIWE SAWA ILA KIKUBWA NI KUONDOA MANYANYASO KWA MAMA ZETU KUWAPA HAKI NA UPENDO WA DHATI NA KUWAHESHIMU DAIMA NA SIO KUSEMA HAKI SAWA NINA HAKIKA HAITAKUJA KUFIKIA NA HAYO NI MOJA KATI YA MAADHIMIO YA KUMPINGA MUNGU KWANI WAKATI ANAYATOA HAYO HAKUKOSEA KUMPA NAFASI HIYO MWANAUME NA KUMACHA MWANAMKE NA NAFASI ALIONAYO NA KAMA ITAWEZEKANA KWA MWANAUME NAE KUTOKA KATIKA UBAVU WA MWANAMKE  BASI HAKI SAWA ITAWEZEKANA NA KAMA MWANAUME NDIE ALIEUMBWA NA MUNGU NA MWANAMKE AKATOKA KATIKA UBAVU HUO NI MBIO ZA MNYONGE AMBAZO HAZITAWASHTUA MATAJIRI AU NDIO MISAFARA YA AKINA MAMBA  NA KENGE WAMO  
 SAMAHANI KAMA KUNA LILIKUA KINYUME NA  MATAKW AYAKO YANGU NI HAYO ILA NAWAHESHIMU AKINA MAMA WOTE DUNIA M NA MAMA YANGU NDIE MAMA WA MFANO UKITAKA KUJUA WASILIANA NA MIMI
MWISHO STEVEN

Wednesday, January 5, 2011

umuhimu wa kula nanasi msimu huu wa mananasi jenga afya.


msimu wa mananasi umeshawadia katika ukanda wote wa pwani. Katika msimu huu bei ya nanasi nalo hushuka na kuwa katika bei ambayo mtu yeyote anaweza kuimudu bila shaka. Hivyo asiyekula mananasi ya kutosha mpaka msimu unaisha, huyo ana hasara kubwa katika afya yake. Ukiacha ukweli huo, tunda hili lina faida ambazo linashawishi kila mtu kulitumia.Faida zinazoweza kupatikana kwenye nanasi ni nyingi ambazo zinaweza kuwa kama kinga na tiba kwa baadhi ya matatizo ya kiafya ambayo pengine yangehitaji mtu kwenda hospitali kupatiwa dawa, tena kwa gharama kubwa. Miongoni mwa faida hizo ni hizi zifuatazo:
KUIMARISHA NURU YA MACHO
Inawezekana karoti ikawa ndiyo inayojulikana na watu wengi kuwa na uwezo wa kuimarisha nuru ya macho, lakini nanasi nalo lina uwezo mkubwa wa kuimarisha nuru ya macho. Utafiti unaonesha kuwa ulaji wa tunda hili na matunda mengine, kiasi cha milo mitatu kwa siku, kunaondoa hatari ya kupungua kwa nuru ya macho kwa asilimia 36 kwa watu wazima.
KINGA YA MWILI
Nanasi linaaminika kuwa miongoni mwa matunda yenye chanzo kizuri cha vitamin C ambayo kazi yake mwilini ni kuupa mwili kinga dhidi ya ‘wavamizi’ mbalimbali (free radicals), ambao wanapoingia mwilini, kazi yao hua ni kuharibu chembembe hai za mwili. Vile vile ‘wavamizi’ hao wanapoweka makazi mwilini, huziba mishipa ya damu na hivyo kusababisha magonjwa ya moyo na mengine mengi, ikiwomo kansa ya tumbo.
Kwa kuongezea, vitamini C inaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili, hivyo kuifanya kuwa kinga ya magonjwa madogo madogo kama vile mafua, kikohozi, homa na maambukizi mengine. Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha vitamin hiyo, bila shaka kinga yako ya mwili itakuwa imeimarika na hivyo utakuwa umejiepusha na maambukizi mbalimbali.
USAGAJI WA CHAKULA
Nanasi lina virutubisho vinavyouwezesha mfumo wa usagaji chakula tumboni kufanya kazi yake ipasavyo, pindi mfumo huu unapowezeshwa kufanyakazi yake vizuri, mtu huweza kupata choo laini na kwa wakati kama inavyotakiwa. Hivyo wenye kula tunda hili kwa wingi hawawezi kusumbuliwa na taizo la ukosefu wa choo. Aidha, kwa mujibu wa tafiti nyingine, nanasi pia lina virutubisho vyenye uwezo wa kupunguza au kuzuia uvimbe tumboni.
Mara baada ya nanasi kumenywa na kukatwa vipande, linatakiwa kuliwa mara moja, iwapo litahifadhiwa kwenye jokofu kwa ajili ya kuliwa baadaye, njia sahihi ya kuhifadhi ni kuliweka kwenye chombo chenye mfuniko (container) ili kuhifadhi virutubisho vyake kwa kipindi hadi cha siku tano bila kupoteza ubora wake, ikiwa pamoja na ladha. 
ILA ZINGATIA HILI
unapokula tunda lolote, zingatia usafi. Osha tunda hadi litakate, nawa mikono yako kwa sabuni au maji moto, kisha shika tunda lako, vinginevyo unaweza kujikuta unakula tunda na vijidudu vya maradhi ya kuharisha na hata kipindupindu.nk 
mwisho wa makala fupi ya nanasi na steven mruma

Friday, December 31, 2010

JE MWAKA MPYA UNAMAANISHA NINI KWAKO JE UNAMALENGO GANI? JE ULITELEZA NA UTAREKEBISHA WAPI?


TAMBUA MWAKA MPYA NA NINI CHAKUFANYA KATIKA MWAKA HUU WA MABADILIKO 2011
Mwaka mpya ni siku ya kwanza ya mwaka na mara nyingi ni sherehe na nafasi ya watu kutakiana heri na baraka za mwaka mpya.

Katika tamaduni mbalimbali nafasi hii ni sikukuu moja au zaidi pasipo na kazi za kawaida.
Tarehe ya mwaka mpya inategemea kalenda yake:
katika sehemu kubwa ya dunia inayotumia kalenda ya Gregori ni 1 Januari
Uajemi, Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Azerbaijan, Turkmenistan na Kashmir husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiajemi kwenye sikukuu ya Nouruz ambayo ni sikusare ya bubujiko inayotokea kati ya tarehe 20 - 21 Machi kwenye kalenda ya Gregori lakini kwao mwezi na mwaka mpya unaanza
Wachina na Wavietnam husheherekea mwaka mpya wakati wa mwezi mwandamu wa pili baada ya solistasi ya majira baridi na hii inacheza kati ya 21 Januari na 21 Februari.
Nchi ya Israeli na Wayahudi husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya kiyahudi kwa jina la rosh hashana ambayo ni siku inayotokea kati ya Septemba na nusu ya kwanza ya Oktoba.
Waislamu na nchi ya Saudia huwa na mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiislamu. Kalenda hii inafuata mwezi tu kwa hiyo sikuu zake huzunguka katika mwaka wa jua.
Sikukuu ya Diwali inasheherekewa na jumuiya kadhaa pia kama mwaka mpya.
Nje ya mahesabu haya kuna kalenda nyingine zisizoanzisha mwaka kwa sherehe. Mifano ni:
mwaka wa shule
mwaka wa biashara ambako hesabu mpya inaanzishwa
mwaka wa kanisa ambayo katika sehemu kubwa ya Ukristo unaanza kwenye jumapili ya Adventi (majilio) ya kwanza. kwa ufupi unaweza ukatambua kuwa mwaka mpya unamaana gani kwako na kwa ujumla wake lazima utambue kila unachopaswa kufanya kila mwaka na hayo ndio malengo yanayo leta mafannikio katika maisha kubali changamoto songa mbele
 NACHUKUA NAFASI HII KUKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA NA MUNGU AUONGOZE MWAKA WAKO UWE NA MAFANIKIO YALIOTUKUKA MBELE YA MUUMBA WAKO ....
 PIGANIA MAISHA YAKO AMINI DAIMA UTASHINDA...... NA USHINDI NI LAZIMA...

Thursday, December 30, 2010

UZINDUZI WA ALBAMU YA TID WAFUNIKA ZOTE ZA 2010 KAMA ULIKOSA BASI USIKOSE ALBAMU HII YA MFANO.


hapa walioshirikishwa katika wimbo uliobeba jina la albamu wa sifai.
mwanaume wa shoka alieonja ladha ya jela
Kama ulikua bado hujui haya nikwambiayo basi chukua hiyo  huyu ni masanii pekee wa mziki wakizazi kipya namaanisha bongo flava ambae amepitia hatua ya kiume ya kuonja japo kidogo ladha ya jela kama kwa akina 50%, lili wayne, akon nk. namkubali mimi pamoja na watanzania na mamilioni duniani kote na kilichofanya mpaka naamua kuandika makala hii ni uzinduzi wa albamu yake mpya ambao uzinduzi huo naweza nikasema ulikua ni moja kati ya uzinduzi bora kuliko yote ndani ya 2010 nilishuhudia wasanii kibao wakimpa shavu wakiwemo akina ngair, Kelvin mshindi wa big braza 2009 na wasanii wengine kibao na staili alionyoa ilikua ni ya kiubunifu na kama ilikua ya kiduku style laniki alizidi ubunifu na kuwa kivutio kikubwa sana ndani ya billicanas hakika kwangu hakuna kama TID AMBAE NDIE NINAYE MZUNGUMZIA HAPA
HISTORIA NA KIMUZIKI HASA ALIPOTOKA…..
TID katika pozi
Jina lake halisi ni Khalid Mohamed a.k.a TID yaani Top In Dar na si yeye anayejiita hivyo bali wapenzi wake TID  alisoma shule ya msingi Bunge na elimu ya sekondari alienda kuipatia pale Shaban Robert iliyopo ndani ya City la Dsm.
Hapa tid anaelezea historia yake kidogo kimuziki hasa alipotokea  |”nanukuu;;; Unajua tangu niko mdogo nilikuwa napenda sana kusikiliza pamoja na kujaribu kuimba nyimbo
mbali mbali....lakini baada ya kuwa mkubwa na kuanza kujishughulisha na shughuli hizi za muziki ndipo wazazi wangu waliponikumbusha kuwa fanii hii nilikuwa nikiipenda sana toka nipo bwana mdogo ile mbaya hapo ndipo nilipojua kuwa kipaji changu kilianzia mbali sana.

.....Ila nilianza kuimba rasmi mwaka 1996 nilipokuwa nipo shule pale Shaaban Robert nikiwa na wenzangu kama David a.k.a Wabaki, Saitana na Dingo Jango ambapo tulianzisha kundi letu lililoitwa Black Gangster na mara nyingi tulikuwa tukiperfom kwenye concerts za kishule na 'Talent Night ' ambazo tulishinda mara kibao. Yap mwaka 1998 tulirekodi albam iliyojulikana kwa jina la Mission Impossible iliyokuwa na nyimbo 12 na ambazo ziliimbwa kwa 'Ngeli' kimombo mzee hahaha. mwaka uliofuata yaani mwaka 1999 nilishirikishwa kwenye nyimbo ya 'Anza wewe' na kundi la Joint Mobb nyimbo ambayo ilikuwepo kwenye albam yao ya 'Kitinda Mimba'. Vilevile nimeshashirikishwa pia kundi la CBM Crew katika Track yao 'My Girl Friend' na mwaka 
hapa makamuzi ya uzinduzi na AY

2000 nikaanza rasmi maandalizi ya Albam yangu.
Mwaka 2001 Crazy GK akanishirikisha kwenye Track yake 'Tutakukumbuka' na 'Malaika' ambazo zote zinapatikana kwenye albam yake inayokwenda kwa jina la 'Nitakupa Nini Mama' na mwaka huo huo nikafeat na kundi la Taqwa ndani ya nyimbo Maovu na Bongo Chelea Pina na Bongo
Chelea pina ambayo inapatikana katika Compilation ya BNa mwaka huo wa 2001 ndio nikaingia mkataba kama Solo Artist na Studio ya Poa Records iliyo chini ya Producer Amit a.k.a Mental ambapo sasa narekodi albam yangu itakayokuja kwa jina la Sauti ya Dhahabu na itakuwa na jumla ya nyimbo 9 kati ya hizo ni pamoja na Mrembo, Zeze, Hii Mic, Ukweli na nyingine ambazo sitazitaja sasa hivi.ongo Records ya mwaka huo  huyu ndie tid kwa kifupi akielezea wapi hasa alipotoka hapa alikua akikaririwa na media moja hapa Tanzania
logo yake muhimu ya kiburudani
NA KAMA UKIKOSA ALBAMU YAKE UTAKUA UMEKOSA MAMBO MENGI SANA NA UTAKUA BADO HUSTAHILI KUWA MDAU WA MZIKI POPOTE DUNIANI PATA KOPY HALISI UINUE MZIKI WA BONGO NA UMUINUE NA TID KATIKA GEMU… PAMOJA SANA
STEVENN MRUMA

Thursday, December 23, 2010

KRISMASI SIKUKUU AMBAYO INAHISTORIA NDEFU SANA NA INAYOPEWA NAFASI KUBWA NA WAUMINI WA KIKRISTO DUNIANI..

NA HII NI HISTORIA FUPI YA SIKUU YA KRISMASI WAPI HASA ILIPOANZIA NA ILITOKANA NA NINI...

Krismasi

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambako Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki  halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma na kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya Sikukuu ya Krismasi.
Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200. Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria (kitabu cha Stromateis I, xxi) alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.
Labda kadirio la tarehe ya Desemba 25 pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya kuzaliwa kwake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.
Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kuchukua nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus". Lakini pengine mambo yalikwenda kinyume, yaani kwamba Makaisari walianzisha sikukuu hiyo halafu wakaipanga tarehe ya Krismasi ili kushindana na Ukristo uliokuwa bado chini ya dhuluma.
Aliyeingiza sikukuu ya Kuzaliwa Jua (Mitra) huko Roma ni Eliogabalus (kaisari kuanzia 218 hadi 222). Baadaye Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273, hatimate ikahamishiwa tarehe 25 Desemba. Wakati wa Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba. (Taz. maandishi yaliyotajwa na Allan S. Hoey katika ukurasa 480 (rejeo 128) wa Official Policy towards Oriental Cults in the Roman Army, Transactions and Proceedings of the American Philological Association (70) 1939, pp 456-481).
Kutoka Roma, uliokuwa mji mkuu wa Dola la Roma, sherehe ya 25 Desemba ilienea kote katika Ukristo.

Wakristo wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki, Waprotestanti, sehemu ya Waorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda 

Habari za Krismasi katika Korani

Korani pia ina habari za kuzaliwa kwake Yesu (nabii Isa).
Sura ya tatu (Al Imran, 42-47) ina habari za tangazo la malaika kwa Bikira Mariamu zinazofanana na Luka 1.
Sura ya 19 (Mariamu, 16-34) inarudia tangazo la malaika kwa Mariamu na inasimulia kuzaliwa kwake Yesu chini ya mti wa mtende, halafu majadiliano kati ya Mariamu na ndugu zake. Mtoto mchanga Yesu akaanza kusema wakati wa kuzaliwa akimtetea mama yake dhidi ya ndugu zake. 
makala hii fupi kupitia vyanzo mbalimbali imehaririwa na steven mruma..