Translate this blog in your favourable language

My pager view

Tuesday, January 8, 2013

MSANII MWINGINE AFARIKI DUNIA BONGO.

     
    
      Kwa habari nilizopata kupitia mitandao asubui ya leo ni ya msanii  nyota wa miondoko ya Mnanda a.k.a Mchiriku, Omari Omar kuwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Habari hizo ziliongeza kuwa asubui hii Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi.

hili ni pigo lingine kwa tasnia ya sanaa hapa nchini kwa tangu kuanza kwa mwaka huu 2013 tayari tasnia ya filamu iliondokewa na aliekuwa msanii maarufu kama SAJUKI aliefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
     lakini kubwa hapa sikuwahi kusikia juu ya kuugua kwa omai omari na kifo chake kimekuwa kama ghafla kwa wengi ambo hatukufahamu kama alikwa anaugua.
   Innallillah Waina Illah Rajiun.
bado nipo katika harakati za kutafuta habari zaidi juu ya taarofa hii na ikapaikana taarifa zaidi juu ya msiba huu zitawajia tena kupitia blog hii. 


LAKINI KUMBUKA KUMUOMBA MUUMBA WAKO HUJUI SAA YA KUANGUKA NI IPI WEWE AU MIMI YAWEZA KUTUKUTA WAKATI WOWOTE LAKINI PIA TUJIEPUSHE NA MOAVU MAANA SIKU IKIFIKA NA UKAITWA WAKATI BADO HUJAJIANDAA MOTO WA JEHANAM UNAKUHUSU.