Credit, Vijimambo Blog.
MBUNGE wa
Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto
Kabwe amesema hawezi kufanya maamuzi magumu ya kutoka ndani ya chama
hicho kwa kile kilichotokea ndani ya chama hicho. Amesema yeye atakuwa
wa mwisho kutoka Chadema na si vinginevyo.
Zitto amekana kuhusika wala kuujua waraka wa siri ambao ndiyo uliosababisha kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama kuunasa waraka huo
"Mimi nimeusikia ule waraka kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu na nilisikitika sana kwanini hukunifikia haraka kwani ningeanza kutekeleza mara moja." alisema Zitto akizungumza.
Huenda
leo watu walitegemea nitafanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye chama;
"Mimi bado ni mwanachama wa Chadema na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye
chama hiki kwa hiyari yangu, nitafanya taratibu zote za chama
kuhitimisha jambo hili mimi sitoki kwenye chama hiki labda wanitoe wao,"
alisema Zitto.
Zitto
alisema anaumia sana anapotuhumiwa kwa kuwa yeye ni binadamu.
"...ninapotuhumiwa naumia ninapoambiwa naujumu chama hiki naumia kwa
kuwa nakipenda chama na nimekitumikia muda mrefu. Aidha aliwataka
viongozi wa Chadema kuacha siasa za uzushi ili kujenga chama himara na
kuwakomboa Watanzania.
"...Sisemi
kama mimi sina makosa ni binadamu nimefanya mambo mengi kwa chama
changu, lakini kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama chetu ni mapambano
ya kukuza demokrasia na ni mapambano ya wanaotaka mabadiliko na
wasiopenda mabadiliko ndani ya chama...mapambano ya wawajibikaji na
wasiopenda kuwajibika ni mapambano ya wanaopenda demokrasia na
wanaokwaza demokrasia." alisema Zitto huku akionesha kusikitishwa.