na Mzava Mbonea kutoka facebook.
SOMA KESI HII YA AGNES DORIS LIUNDI YA MWAKA 1978 ALIVYO WAUA WATOTO WAKE 3 NA KUBAKIZA TAJI LIUNDI PEKEE, ENDELEA KISHA TOA MAONI .
Tukio lenyewe lilitokea hapo majira ya asubuhi mnamo Februari 21, 1978. Ni baada ya kuambiwa mumewe wakati anaenda kazini kwamba akirudi asimkute hapo nyumbani, na kama akimkuta, atamtoa hapo nyumbani kwake uchi. Alikuwa na watoto wao wanne hapo nyumbani. Baada ya mumewe kuondoka, na yeye aliondoka na gari kuelekea mjini ambapo alinunua chupa kadhaa za sumu ya kuulia wadudu.