baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mihani ya taifa |
ufaulu ulikuwa ni kama ifuatavyo.
watahiniwa laki mbili na elfu 25 sa.wa na asilimia 53.37 wamefaulu huku kati yao wasichana ni elfu 90 na 885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni laki moja na elfu 34 sawa na asilimia 57.51.Shule ya sekondari ya wasichana ya St. Francis Mbeya imeongoza kwa shule kumi zilizofanya vizuri, ambapo katika wanafunzi waliofaulu vizuri sana wameongozwa na Moses Andrew Swai kutoka shule ya sekondari ya Feza iliyopo jijini Dar es salaam.
lakini ukiangalia shule mia bora hakika huwezi kukuta shule ya sekondari ya kata wala ukiangalia zilizo felisha sana huwezi kukuta shule binafsi hii ni kwasababu ya mazingira ya elimu bora inayotolewa na shule hizo na kama serikali ingeboresha shule angalau kwa asilimia 50 labda tungefika mbalia sana. lakini hali ni tete sana kuko vijijini....
nini chanzo cha wanafunzi wote hao ambao hawana tena muustakabali wa maisha yao ya shule?
shule za kata ni... |
1. Sera mbovu kabisa za elimu hasa ya kujenga sekondari nyingi bila kuwa na uwezo wa kuzihudunmia.....
hili ni tatizo kubwa sana ambalo nimeliona niliwahi kuwa mwalimu wa shule moja ya kata kama mwalimu wa muda ikafika kipindi walimu wako semina inabidi watafutwe wanafunzi waliomaliza kidato cha nne wakafundishe katika ile shule. shule zipo nyingi walimu wachache vitendea kazi hakuna kama vitabu pamoja na maabara kwaajili ya masomo ya sayansi. hatawezi kupata mafanikio ya elimu kwa kuweka majengo mengi na kisha wanasiasa wanajisifu kuwa wanafunzi wengi wameingia sekondari kisha hawajui kama wanasoma au la huu ni ujinga wa makusudi sio kwamba hawajui....
ni wangapi wanapata fursa hii ya kusoma na kufaulu? |
nimekutana na changamoto nyingi sana katika maeneo ya vijijini ambayo nina uzoefu nayo sana unakuta shule ya sekondari wanafunzi wanenda shule mda wanaoutaka kwasababu walimu hawafiki kazini kwa wakati na wanaweza kuondoka kituo cha kazi mda atakaojisikia na hili linasababishwa sana na wazazi na wanafunzi bila kusahau wanasiasa hasa madiwani
3. Utovu wa nidhamu shuleni hasa suala la mapenzi..
katika mabo ya ajabu kabisa suala la mapenzi shuleni limekuwa jambo la kawaida sana na wala hata ikatokea walimu wakawa wanafahamu kuwa kuna miongoni mwa wanafunzi wanajihusisha na suala la mapenzi hakuna hatua yoyote inayochukuliw a kuondoa hali hiyo ama kuwapa adhabu kulingana na sheria za shule... lakini baya zaidi walimu wengi kuwa na mahusiano na wanafunzi pamoja na wafanyabiashara wakubwa mabo pia wanachangia sana mimba shuleni.
hakuna jipya san ufaulu umeongezeka shule binafsi. |
wanafunzi wamesoma kata na kijiji kimoja kisha anaenda sekondarui palepale hewezi kupata changamoto za kimaisha na kubadili mawazo kwa kuwa na kabila ama watu wa aina tofautoi na uliozoea kwani ujinga aliotoka nao shule ya msingi anaingia nao sekondari na wajinga wenzie walewale wa mtaani anakutana nao na hakika kusoma hapa inakuwa ishu ni bora kungekua na karatasi au fomu maalu amabyoi mzazi atajaza kama atakuwa na uwezo wa mtoto wake akipelekwa wilaya nyingine au mkoa mwingine atamudu gharama ili watoto hawa wapelekwe maenieo tifauti kubadili mawazo na kubadili mfumo wa maisha yao..
ukimaliza four kula zako bata basi |
Makala hii kama kawaida imeandikwa na Steven Mruma bila ushawishi wa mtu yeyote na naupongeza mgomo wa madaktari unaoendelea maeneo mbalimbali hapa Tanzania. Malizeni madokta walimu najua mnajiandaa bia kusahau idara mbalimbali kama za sheria watendaji nk....
MWISHO