Translate this blog in your favourable language

My pager view

Monday, December 20, 2010

kupatwa kwa mwezi na jua [solar and lunar eclipse] matukio ya kawaida sasa duniani

leo itatokea kupatwa kwa mwezi usiku na hili ni kutoka kwa watbiri wa hali ya hewa 

 katika habari za kitabiri leo jumatatu kutatokea kupatwa kwa mwezi na hii imenifanya nikumbushie matukio haya ambyo yalitabiriwa kama ndio dalili za mwisho wa dunia na hali hii ya kupatwa kwamwezi ni yakawaida kabisa hapa duniani...

Kupatwa kwa jua kunatokea wakati mwezi unafunika jua. Tokeo lake ni kupungua kwa jua hadi kutoonekana tena na kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu.  Misingi ya kupatwa kwa jua
Kupatwa kwa jua kunatokea kama dunia, mwezi na jua zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua. Katika hali hiyo kuna kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia. Kivuli hiki hakifuniki dunia yote. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua             
Aina za kupatwa kwa jua
Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa jua.
  • kupatwa kabisa: jua lapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.
  • kupatwa kipete: mwezi huonekana mdogo kuloko jua. Kwa hiyo duara ya kung'aa ya jua ni kubwa kuliko duara ya mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete.
  • kupatwa kwa jua kisehemu: Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu hona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. Wakitazama jua kwa filta kwa mfano kioo kilichopakwa dohani katika moshi ya mshumaa huwa wanaona sehemu ya duara ya jua imefunikwa. 
KUPATWA KWA MWEZI
H hutyokea pale dunia inapokua katikati ya jua na mwezi na kufanya mwezi ushindwe kuakisi mwanga kutoka kwenye jua ikumbukwe kua mwezi hupata ama huakisis mwanga wake kutoka kwenye jua sasa dunia inapokua katikati mwanga wa jua haufiki katika mwezi na kusababisha mwezi kua na giza na hii haichukui muda mrefu kisha hali huwa kama kawaida na matukio haya hutokea mara kwa mara sasa duniani na limekua kama jambo la kawaida kabisa