Translate this blog in your favourable language

My pager view

Thursday, April 5, 2012

NINI CHANZO CHADEMA KUPOKWA JIMBO LA ARUSHA MJINI NA MAHAKAMA?


Katika hali ambayo awali haikutegemewa na wanachi wengi majira ya saa nne asubuhi mahakama kuu mjini arusha ilimuondoa mbunge wa arusha mjini Godbless lema kwa kile kilicho daiwa kuwa ni kutumia lugha ya matusi katika kampeni zake na kuongea lugha za uchochezi ambazo zingeweza kuhatarisha amani ya nchi kitu ambacho ni kinyume na sheria. wengi walijiuliza kama kulikuwa na mono wa mtu lakini kwa mujibu wa mahakama katika mikutan zaidi ya 60 ya kampeni ya Godbless Lema mikutano Nane (8)  alivunja sheria na alitumia lugha za uchochezi, kuna taarifa zilizokuwa zimezagaa baadhi ya mitaa eti aliondolewa katika nafasi hiyo kwasasababu alidanganya uma kuhusu masomo yake ikiwemo vyeti nk.
 lakini baada ya majibu na hukumu ya mahakama alivuliwa ubunge kwasababu ya kutumia lugha chafu na za uchochezi katika kampeni zake wakati akigombea kuingia bungeni mwaka 2010. na wakati huo huo Maandamano ya wafuasi na wanachama wa CHADEMA wakimsindikiza "Aliyekuwa mbunge wao" wa Arusha mjini ndugu Godbless Jonathan Lema kuelekea viwanja vya Ngarenaro majira ya saa 8 na dakika 15 ambapo hatimaye alihutubia wananchi. Mahakama imetengua ubunge wa Lema kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM.


Godbless Jonathan Lema amekubali uamuzi wa mahakama na amesema haina haja ya kukata rufaa isipokuwa ATASHINDA TENA kiti hicho katika uchaguzi mdogo utakaoandaliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi. kwani bado anaruhusiwa kugombea tena kiti hicho cha ubunge na kwataarifa isiyokuwa rasmi ikulu imekataa kuhusika kwa kuvuliwa kwa ubunge kwa aliyekuwa mbunge wa chadema Godbless lema.