Translate this blog in your favourable language

My pager view

Tuesday, May 1, 2012

YALIYOJIRI KATIKA SIASA MBUNGE HUYU NAYE CHALI.sasa zamu ya CCM.



Katika hali ambayo ilidhaniwa na wengi kabla ya hukumu ya aliyekuwa mbunge wa sumbawanga mjini Aeshi Hillary avuliwa rasmi ubunge na sasa jimbo hilo lipowazi, hii ni kutokana na malalamiko ya mgombea mwenzake katika uchaguzi wa 2010 kupitia CHADEMA kumfungulia mashtaka kwa kukiuka sheria za uchaguzi, ikiwemo kutokea kwa fujo na kashfa mbalimbali za rushwa akiongea kupitia vyombo vya habari mbunge huyo ameahidi kukata rufaa na amesema kuwa anashangazwa sana na maamuzi ya mahakama kwa kumtia hatiani kufuatia wafuasi wake kufanya vurugu ambazo ndizo zimepelekea kuvuliwa ubunge pia amedai kuwa huwezi kumtambua mfuasi wa chama kwa fulana aliyo vaa hivyo mahakama haikuwa na uhakikwa wa kuwa waliofanya fujo hizo walikuwa ni wafuasiwa CCM kwani huwezi kumtambua mfuasi wa chama kwa fulana aliovaa bali utamtambua kwa kadi ya chama na sio vinginevyo, pia mbunge huyo hakubainisha wala kuongelea tuhuma za rushwa ambazo pia zilichangia kumvua ubunge na ikiwemo kutuhumiwa kutoa rushwa ya baikeli pikipiki na vitu mbalimbali kwa sharti la kupigiwa kura. mengi zidi tutayapta hasa baada ya mbunge alievuliwa ubunge kukata rufaa. kwasasa jimbo hilo la sumbawanga mjini lipo wazi huku CHADEMA wakichekelea kwani kunauwezekano mkubwa wa kuchukua jimbo hilp haya yamebainishwa jana katika sherehe fupi ya kushangili ama kupongeza uamuzi wa mahakama kwa kumvua ubunge mbunge huyo.