Translate this blog in your favourable language

My pager view

Wednesday, October 17, 2012

KUKOJOLEA MSAHAFU = KUANDAMANA, KUHARIBU MAKANISA, KUHARIBU MAGARI?

        

gari ya clouds media ilioharibiwa katika maandamanoya waislamu
        Wakati maandamano ya waislamu yametokea nilitumia muda mwingi sana kwa ajili ya kuangalia na kuchambua pamoja na kutathmini yaliyotokea kwa wenzetu waislamu na kwa upande pia wa wakristo. Awali ya yote napenda kutoa pole kwa waislamu wote kwa kitendo kilichofanywa na kijana Emmanuel Kwa kukojolea msahafu ni kitendo cha udhalilishaji wa dini, hii ni bila kushau kuwa kila mtu anapaswa kuheshimiwa katika kile anachokiamini hasa katika upande wa dini. Lakini pia nitoe pole kwa wakristo ambao makanisa yao yalivunjwa na vurugu na maandamano ya waislamu haikuwa busara kuvunja lakini wanapaswa kusamehewa bure hasa ukizingatia aina ya waliofanya vurugu hizo ni akina nani na wana itkadi gani. Kabla sijagusia maandamano na vurugu za mbagala napenda nirudi kidogo nyuma. Hapa nazungumzia maandamano ya waislamu Zanzibar ambayo pia yaliandamana na kuvunjwa kwa makanisa pamoja na baa. Mei 26 2012 kisiwani Zanzibar maeneo ya darajani palitokea fujo iliofanywa na kikundi cha uamsho kwa shinikizo la kutaka kiongozi wao atolewe mahabusu alipokuwa anashikiliwa na polisi kwa kosa la kufanya mikutano ya hadhara bila kibali. Pili zilikuwa ni harakati za kupinga muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Sasa napenda ufananishe mantiki ya mdai ya wafanya vurugu hao na kisa cha kuvunja makanisa na baa na kufanya fujo kufunga barabara nk. Je ndio lilikuwa suluhisho la walichokuwa wanakitaka?

. Mwenye akili na afahamu.  Katika hayo yote ningependa sana ufuatilie tene kwa makini sana lile tukio la Zanzibar katika mitandao na kasha fananisha madai ya waislamu hao na kuchoma baa na makanisa. Mtazamo wangu.  1.    Lilikuwa ni jambo la kudhalilisha na kufedhehesha kwa kuvunja makanisa wakati hawakua chanzo au sio walioiunganisha Zanzibar na Tanganyika na waasisi wa muungano wanajulikana mngeenda kuvunja nyumba zao. 2.     Lakini pia hao mliovunja makanisa yao sio waliomkamata kiongozi wenu anashikiliwa na polisi kama mngekuwa na hasira ya kweli mngeenda kuvunja nyumba za polisi na vituo vyao. 3.    ILIKUWA NI DHARAU KUBWA SANA KUVUNJA MAKANISA NA BAA KWANI ILIKUWA DHAHIRI MNAFANANISHA MAKANISA NA BAA HII NI DHARAU NA NAPENDA KUILINGANISHA NA KITENDO CHA EMMA KUKOJOLEA MSAHAFU. ( msiwe hodari kuona vibanzi katika macho ya wenzeni wakati macho yenu yanamaboliti) na kumbuka kumhukumu mtu wakati MUNGU yupo ni kutaka kufanya kazi ya MUNGU wakati yeye anajua kila kitu zaidi ya mchanga wa bahari je nyie mnajua mangapi kumshinda MUNGU?     Ieleweke kuwa kila dini inathamini kile wanachokiamini yalipovunjwa makanisa Zanzibar hakuna aliejibu mapigo alilia na sheria ifuate mkondo kwa kua dini zinaitambua mamlaka ya kisheria na kiserikali.     

Sasa napenda turud katika tukio husika la mbagala kama hujafahamu mengi yaliyptokea naomba soma katika mtandao huu habari ya iliopita kabla yah ii na pia utaona picha za tukio zima kwa ajili ya kuelewa na kupata ushahidi wa hiki ninachokisema. Kwanza napenda kulaani kitendo cha Emmanuel kukojolea msahafu hakikua kitendo cha kiuungwana haijalishi sana kama ulikuwa mjinga kiasi gani chamsingi kilichofanyika hakikua kitendo kizuri na kinapaswa kupingwa kwa nguvu. Lakini pia nipende pia kuaani kitendo cha waislamu hao walioandamana kwa kuvunja makanisa ilhali sheria ipo na tayari hatua za kisheria shilisha anza kuchukuliwa kwani kijana huyo tayaria alikuwa mikononi mwa polisi.    Lakini pia napenda tu kuwa wazi na kusema ukweli waislamu mlioandamana na wale wote mnaounga mkono kitendo cha kuvunjwa kwa makanisa na kufanya vurugu na kuharibu na kuchoma magari pamoja na kufunga njia kwa mtindo mnaoenda nae mnadanganyika na ni kufilisika kimawazo na hilo sio sulihisho la matatizo yenu. Msiige sera za mashariki wengi wao si waislamu kama nyie ni tofauti kama hauamini fatilia sera za alshababu madhehebu ya shia na suni na kasha rudi jiangalieni na waislamu wa Tanzania.          Yote yaliyotokea mlipaswa kiacha sheria ifuate mkondo wake sambamba na kulaani kitendo kile. Kwa kufanya fujo zile mimi naona ilikua ni sera ya kijinga ambayo mwisho wa siku imeishia kuwatia hatiani wengi ikiwemo na wasiokua na hatia. Na pia mmetia hasra ambayo sheria hiyohiyo mlioshindwa kuiacha ichukue mkondo italazimu kuigharamia.        Matajiuliza kwanini mimi naona ni sera ya kijinga na ni kufilisika kimawazo ninasema hayo kwa mambo makuu yafuatayo:- 1. 

 Aliekojolea msahafu tayari alikuwa mikononi mwa polosi kama mliona sheria haiwezi kuchua mkondo kwanini msivunje mahakama na poilisi kwa kuwa wameshindwa kufanya kazi? Mnakimbilia kuvunja makanisa ambayo hata huyo kijana hayajui na hasali katika makanisa hayo makanisa yaliovunjwa ni Anglikana Sabato na roman catholic sasa huyu kijana anasali katika makanisa haya yote?  2.    Huyu kiana alikuwa na miaka 14 na najua mnajua fika kua huyu ni motto hata kama angekua na akili kiasi gani neon na sifa kama mtoto bado anabaki nalo na hili linadhihirisha upumbavu na ujinga wake sasa watu wazima mnatakiwa kukaa chini na kutafakari mnataka kushindana na mtoto sijui kama nikisema mmefilisika kimawazo na ule ulikuwa ni ujinga sawa na ujinga wa mtoto huyo aliekojalea msahafu hapo sioni tofauti