Rais Kikwete alifika katika makaburi hayo mapema kabla ya mwili wa marehemu kuwasili na kukaa katika viti vilivyokuwa vimeandaliwa maalum kwa ajili yake.
Rais Kikwete alimfariji Baba mzazi wa marehemu mzee Kilowoko pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifwamba.
Msanii huyo wa Filamu nchini alifariki Dunia juzi alfajiri kwenye Hospitali ya Taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.Sajuki ameacha mjane na mtoto mmoja, wa miezi tisa
Baba mzazi wa marehemu Sajuki,mzee Kilowoko akiweka udongo kwenye kaburi la mwanaye.Picha zote na Jackson Odoyo