RAIS Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya Watanzania katika mazishi ya
aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Juma Kilowoko maarufu kama
(Sajuki), katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete alifika katika makaburi hayo mapema kabla ya mwili wa
marehemu kuwasili na kukaa katika viti vilivyokuwa vimeandaliwa maalum
kwa ajili yake.
Rais Kikwete alimfariji Baba mzazi wa marehemu mzee Kilowoko pamoja
na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifwamba.
Mbali na Rais Kikwete kushiriki katika maziko hayo pia alikuwepo Meya
wa Jiji la Ilala Jerry Silaa pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe.
Msanii huyo wa Filamu nchini alifariki Dunia juzi alfajiri kwenye Hospitali ya Taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.Sajuki ameacha mjane na mtoto mmoja, wa miezi tisa
1 comment:
Great blog! Is your theme custom made or did you download it from
somewhere? A design like yours with a few simple adjustements would really
make my blog jump out. Please let me know where you got your theme.
Cheers
my blog post :: dating online (http://bestdatingsitesnow.com)
Post a Comment