Translate this blog in your favourable language

My pager view

Wednesday, February 8, 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HALI YA SHULE ZA KATA HALI BADO NI MBAYA SANA, ZAZIDI KUFELISHA.




 WAKATI NAJARIBU KUFATILIA MATOKEO YA SHULE MBALIMBALI YA SHULE ZA SEKONDARI KWA MWAKA 2011 MITIHANI AMBAYO ILIFANYIKA MWAKA JANA MATOKEO YAKE YAMETOKA NA YAMEKUWA NA HALI MBAYA HASA KWA SHULE ZA KATA AMBAZO NDIZO ZIPO KATIKA HALI MBAYA SANA NILIJARIBU KUANGALIA NA MATOKEO YA SHULE BINAFSI HALI HAIKUWA MBAYA SANA KAMA AMBAVYO IMEKUWA KATIKA HALI HIYO YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUWA MBAYA SNA BADO NARUDISHA LAWAMA KWA SERIKARI HASA BARAZA LA MITIHAANI PAMOJA NA WIZARA HUSIKA KWA KUFANYA MABADILIKO YA KIJINGA NA KUSABABISHA WANAFUNZI WENGI KUPOTEZA MUELEKEO WA MAISHA HASA WALE AMBAO WANASOMA SHULE ZA KATA AMBAO WENGI MAISHA YAO NI DUNI SANA.
kama hanuna advance wangefaulu wengi wangeenda wapi?
NA HAKIKA WIZI UJAMBAZI UKOSEFU WA AJIRA ONGEZEKO KUBWA LA MAHARAMIA LINAKUJA TANZANIA, KWANI WANAFUNZI HAO AMBAO HUFELI KIDATO CHA NNE WENGI WAO HAWANA UWEZO WA KUFANYA LOLOTE ZAIDI YA KWENDA KUSHINDA VIJIWENI NA KUJIFUNZA UHUNI NA WIZINA KATIKA HILI LAZIMA TUIANGALIE ELIMU YA TANZANIA.

ZIFUATAZO NI MOJA KATI YA SERA MBOVU NA ZA KIJINGA NILIZOWAHI KUSHUHUDIA AMBAYO IMEFANYA MATOKEO HAYA KUWA MABAYA KUPINDUKIA...

      1. KUFUTA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI NA KURUHU WANAFUNZI WABOVU KUSONGA MBELE...
watapendeza mavazi sio elimu kwa sera hizi mbovu
 KATIKA SERA ZA KIJINGA KATIKA WIZARA YA ELIMU KUSHUHUDIA HII NI MOJA KATI YA SERA MBAYA AMBAYO NDIO INAGHARAIMU MAISHA YA KUFELI YA WANAFUNZI WENGI SANA.  NILISHAWAHI KUFUNDISHA TEMPO KATIKA SHULE MOJA YA KATA KIPINDI CHA NYUMA NA KUSHUHUDIA HALI MBAYA ZAIDI KUTOKEA WANAFUNZI HAWASOMI NA WALA HAWANA WASI WASI KABISA NA WALA HAKUNA KUSHTUSHWA KAMA WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA MBELENI..
2.  MABADILIKO YA MARA KWA MARA YA MTAALA WA ELIMU AMBAO HUANZIA SHULE ZA MISINGI.
Ndalichako kazini
 HUKU NI KUKOSA UMAKINI NA NDIO MAAN AKUNA SERA MOJA YA WAZIRI MUNGAI AMBAYO NA ILAANI MPAKA KUINGIA KABURINI KWA KUFUTA MASOMO YA BIASHARA NA KILIMO NA HILI KUNIHARIBIA HATA MIMI MABAYE NILIKUWA NA MALENGO YA KUSOMA MASOMO YALIYOFUTWA HAITOSHI AKAFANYA PHYSIKIA NA CHEMIA KUWA SOMO MOJA AMBOAYO NDIO ERA MBOVU KUWAHI KUTOKEA DUNIANI. HUWEZI KUCHANGANYA KIFO NA USINGIZI

USHAURI WANGU KWA SERIKALI
hatari hii inakuja
 IMEFIKA WAKATI RAIS ANAPOCHAGUA WAZIRI WA ELIMU PAMOJA NA MAKATIBU NA WAFANYAKAZI WA WIZARA HUSIKA WAANGALIE WATU AMBAO WANA TAALUMA YA UALIMU KATIKA NGAZI MBALIMBALI AMBAO NDIO WANAJUA  NA WANAKUTANA NA CHANGAMOTO NYINGI SANA ZA KIELIMU NA HAO NDIO WANAOJUA CHANGAMOTO ZA ELIMU HASA VIJIJINI NA HILI LINAWEZA KUSAIDIA KIDOGO KUBORESHA ELIMU YA TANZANIA SIO KILA WAZIRI ANALETA BANGE ZAKE KILA AKITAKA KUFANYA KITU ANAKURUPUKA NA KUWEKA VITU VYA KIPUUZI NA MWISHO WANAHARIBU ELIMU YA TANZANIA NA SIJUI HAWA WALIOFELE NA HAWANA UWEZO TUWAPELEKE WAPI MANA MAJAMBZI WAHUNI VIBAKA NA MACHANGUDOA BILA SHAKA WATAONGEZEKA KWANI NAJUA FIKA HAWA HAWANA PAKWENDA.

ANGALIZO NA NIONAVYO MIMI.
yaleyale kichwa epty sera mbovu
KUFELI HUKU INAWEZEKANA NI JANJA YA SERIKALI KUONDOA LAWANA ZA WANAFUNZI WATAKAO HITAJI KUINGIA KIDATO CHA TANO KWANI KULINGANA NA
 IDADI YA WANAFUNZI WALIOMALOZA NA UWEZO WA SHULE ZA KIDATO CHA TANO NA SITA NAJUA KAMA WAKIFAULU 60% HAWATOSHA NA PIA WAKIFAULU KIWANGO CHA VYUO HAPATAKUWA NA NAFASI PIA ZA KUWAWEKA ACHILIA MBALI KUWAPA AJIRA KWA USHAHIDI HUU WALIMU WALIOMALIZA MWAKA JANA WAMEKAA NYUMBANI MPAKA MWEZI WA KWANZA NA WAPILI MWEZI HUU NDIO WAMEPATA AJIRA IKIWA NI DALILI ZA KUTOKUWA NA PESA ZA KUWAAJIRI NDIO MAANA NAHISI KUNA UJANJA UJANJA HAPA ILI KUOKOA HAYO MACHACHE NILIO YATAJA KWANI WAPINZANI WENGI SI VIJANA TENA WENGI WAO WALIOSOMA LEO WA KIJIJINI ATAJUA NINI KAMA ATAISHIA NA KIFORM FOUR CHAKE CHENYE FAIL AU IV YA 29 NAKUENDELEA . HAPA NAKUMBUKA KAULI YA FUNIKA KOMBE.......... APITE KAMA SIO BORA PUNDA AFE ILA MZIGO UFIKE..... WAO KAZI YAO KUONGEZA POSHO ZAO HAWAJALI UBINADAMU WAO NI PEASA NA MASLAHI BINAFSI NDIO MAANA WATANZANIA WENGI WANAKUFA KWA MGOMO WA MADAKTARI LAKI WAO WALIKATAA HATA HOJA YA MNYIKA KUJADILI MGOMO HUO HUU NI UJINGA WA WAZI TUNAOFANYIWA WATANZANIA AMKA NA KWA NIA MOJA HATA NIKIUGUA MIMI AU YEYOTE SIJALI MGOMO WA MADAKTARI UDUMU KABISA NA NAUNGA MKONO KWA 100%..... VITA MBELE MAUTI NYUMA...

MAKALA HII IMEANDALIWA NA STEVEN MRUMA. BILA MSAADA WALA USHAURI WOWOTE KUTOKA KWA MTU YEYOTE.. KWA MASWALI MAONI 0719507240.... steven.mruma@gmail.com au facebook search steven mruma.