HATIMAYE LULU AZUNGUMZA ASEMA HAKUMSUKUMA KANUMBA Baada ya kugoma kutoa maelezo kwa takribani siku nzima ya jana, mwanadada Lulu hatimaye amezungumza na polisi na kuelezea kilichotokea baina yake na marehemu Steven Kanumba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema Kanumba alikufa kutokana na u...gomvi uliotokea kati yake na rafiki yake wa kike Lulu. "Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo (jana) majira ya saa tisa usiku, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ugomvi kati yake na rafiki yake wa kike anayejulikana kwa jina la Elizabeth Michael 'Lulu' mwenye umri wa miaka 18. Alisema kabla ya ugomvi huo kutokea kati yao wakiwa chumbani, simu ya Lulu iliita na akaamua kutoka nje kupokea kitendo kilichomuudhi Kanumba. Kamanda Kenyela alisema Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti akitaka aelezwe kwanini alitoka nje kupokea simu huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.
Aliongeza baada ya Lulu kuona Kanumba akimfuata aliamua kukimbia kutoka nje ya geti , lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na kumrudishwa ndani. Kamanda Kenyela, alisema Kanumba akiwa amemshikilia waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Hata hivyo, alisema haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu anadi kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba. Kamanda huyo alisema Lulu anaeleza kuwa baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini. Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Kanumba alikuwa amekunywa Whisky (pombe kali) aina ya Jacky Daniel, hata hivyo, bado wanachunguza zaidi kujua kama kweli Kanumba alilegea tu na kuanguka, ama alipigwa na kitu kizito kichwani au alisukumwa kwa nguvu na kumfanya aangukie kisogo. “Uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani kwa tuhuma za mauaji,” aliongeza Kamanda Kenyela.
Steven kanumba aliyefikwa na mauti usiku wa kuamkia jumamosi atazikwa kesho jijini dar es salam katika makaburi ya kinondoni kama amabvyo familia na wadau walivyopendekeza azikwe jiji dar. Kamati ya mazishi inayoongozwa na Mtitu ilitoa taarifa ya ratiba hiyo na ratiba hiyo iakuwa ni kama ifuatavyo.
RATIBA KAMILI.
Mwili wa marehemu Steven Kanumba
utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili saa 2:30
asubuhi. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi
hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea
itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.
Wito
unatolewa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi,
wakijipanga kando ya Barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi
ili wautolee heshima mwili wa Kanumba wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.
Saa 3:30 asubuhi,
mwili wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na
mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao
kabisa atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
Mohamed Gharib Bilal.
Saa 4:00, itakuwa ni muda wa kusoma
Misa ambayo itachukua dakika 60, saa 5:00 kitakuwa kipindi cha salamu
kutoka kwa watu mbalimbali.
Saa 6:00 mchana, ratiba ya kumuaga
Kanumba itaanza mpaka saa 9:00 alasiri na baada ya hapo, utakuwa wakati
wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club mpaka Makaburi ya
Kinondoni, msafara ukipita Barabara ya Tunisia, utakatisha Barabara ya
Kinondoni kuelekea makaburini.
Saa 10:00 alasiri, mazishi yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.
Kamati ya Mazishi inatoa wito kwa watu
watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu Kanumba, kuja na maua
ili kumuaga kwa heshima.
Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani
aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake
ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.
K.N.Y GABRIEL MTITU
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI