gari ya clouds media ilioharibiwa katika maandamanoya waislamu |
. Mwenye akili na afahamu. Katika hayo yote ningependa sana ufuatilie tene kwa makini sana lile tukio la Zanzibar katika mitandao na kasha fananisha madai ya waislamu hao na kuchoma baa na makanisa. Mtazamo wangu. 1. Lilikuwa ni jambo la kudhalilisha na kufedhehesha kwa kuvunja makanisa wakati hawakua chanzo au sio walioiunganisha Zanzibar na Tanganyika na waasisi wa muungano wanajulikana mngeenda kuvunja nyumba zao. 2. Lakini pia hao mliovunja makanisa yao sio waliomkamata kiongozi wenu anashikiliwa na polisi kama mngekuwa na hasira ya kweli mngeenda kuvunja nyumba za polisi na vituo vyao. 3. ILIKUWA NI DHARAU KUBWA SANA KUVUNJA MAKANISA NA BAA KWANI ILIKUWA DHAHIRI MNAFANANISHA MAKANISA NA BAA HII NI DHARAU NA NAPENDA KUILINGANISHA NA KITENDO CHA EMMA KUKOJOLEA MSAHAFU. ( msiwe hodari kuona vibanzi katika macho ya wenzeni wakati macho yenu yanamaboliti) na kumbuka kumhukumu mtu wakati MUNGU yupo ni kutaka kufanya kazi ya MUNGU wakati yeye anajua kila kitu zaidi ya mchanga wa bahari je nyie mnajua mangapi kumshinda MUNGU? Ieleweke kuwa kila dini inathamini kile wanachokiamini yalipovunjwa makanisa Zanzibar hakuna aliejibu mapigo alilia na sheria ifuate mkondo kwa kua dini zinaitambua mamlaka ya kisheria na kiserikali.
Sasa napenda turud katika tukio husika la mbagala kama hujafahamu mengi yaliyptokea naomba soma katika mtandao huu habari ya iliopita kabla yah ii na pia utaona picha za tukio zima kwa ajili ya kuelewa na kupata ushahidi wa hiki ninachokisema. Kwanza napenda kulaani kitendo cha Emmanuel kukojolea msahafu hakikua kitendo cha kiuungwana haijalishi sana kama ulikuwa mjinga kiasi gani chamsingi kilichofanyika hakikua kitendo kizuri na kinapaswa kupingwa kwa nguvu. Lakini pia nipende pia kuaani kitendo cha waislamu hao walioandamana kwa kuvunja makanisa ilhali sheria ipo na tayari hatua za kisheria shilisha anza kuchukuliwa kwani kijana huyo tayaria alikuwa mikononi mwa polisi. Lakini pia napenda tu kuwa wazi na kusema ukweli waislamu mlioandamana na wale wote mnaounga mkono kitendo cha kuvunjwa kwa makanisa na kufanya vurugu na kuharibu na kuchoma magari pamoja na kufunga njia kwa mtindo mnaoenda nae mnadanganyika na ni kufilisika kimawazo na hilo sio sulihisho la matatizo yenu. Msiige sera za mashariki wengi wao si waislamu kama nyie ni tofauti kama hauamini fatilia sera za alshababu madhehebu ya shia na suni na kasha rudi jiangalieni na waislamu wa Tanzania. Yote yaliyotokea mlipaswa kiacha sheria ifuate mkondo wake sambamba na kulaani kitendo kile. Kwa kufanya fujo zile mimi naona ilikua ni sera ya kijinga ambayo mwisho wa siku imeishia kuwatia hatiani wengi ikiwemo na wasiokua na hatia. Na pia mmetia hasra ambayo sheria hiyohiyo mlioshindwa kuiacha ichukue mkondo italazimu kuigharamia. Matajiuliza kwanini mimi naona ni sera ya kijinga na ni kufilisika kimawazo ninasema hayo kwa mambo makuu yafuatayo:- 1.
Aliekojolea msahafu tayari alikuwa mikononi mwa polosi kama mliona sheria haiwezi kuchua mkondo kwanini msivunje mahakama na poilisi kwa kuwa wameshindwa kufanya kazi? Mnakimbilia kuvunja makanisa ambayo hata huyo kijana hayajui na hasali katika makanisa hayo makanisa yaliovunjwa ni Anglikana Sabato na roman catholic sasa huyu kijana anasali katika makanisa haya yote? 2. Huyu kiana alikuwa na miaka 14 na najua mnajua fika kua huyu ni motto hata kama angekua na akili kiasi gani neon na sifa kama mtoto bado anabaki nalo na hili linadhihirisha upumbavu na ujinga wake sasa watu wazima mnatakiwa kukaa chini na kutafakari mnataka kushindana na mtoto sijui kama nikisema mmefilisika kimawazo na ule ulikuwa ni ujinga sawa na ujinga wa mtoto huyo aliekojalea msahafu hapo sioni tofauti
. 3. Ilitakiwa mtambue ya kuwa kuwa kisa juu ya kisa ni visa tukio la Zanzibar lilisababisha kuvunjwa kwa makanisa wakti kisa cha maandamano na vujo hazikuhusiana na itikadi za kidini kwa moja kwa moja. Lakini makanisa yalivunjwa tena ngalia tukio la mbagala pamoja kama kisa kinaendana na itkadi za kidini lakini walivunja magari ya waandishi wa habari ambao ndio waliwasaidia mpaka kila mtanzania amejua kilichotokea na kukilaani. Sasa jiulize gari lilikufanya nini l;ile gari la clouds media wewe uliendamana au wewe ambae unaunga mkono vujo na vurugu zile? Kisa cha dini mnagombana na mpaka waandishi wa habari wapi na wapi. 4. Sio mara moja kuwaona baadhi ya waislamu kukurupuka kwa kuchukua maamuzi ya kijinga na yasiyokuwa na tija kwa na kwa wengine kumbuka yale ya mwembe chai, kumbuka wale wa Tanga waliokuwa wanandamana kutaka mahaka ya kadhi, kumbuka yale vurugu za Zanzibar wakati wa ajali ya meli miezi kadhaa iliopita kati yao na pilisi. Halafu tafuta maandamano ya wakristo au vurugu za wakristo hata za kupigana wao kwa wao achilia mbali kuwafanyai fujo waislamu. 5. Dini ya kislamu kitafsiri ni dini ya amani je ni amani ipi hiyo kama kuna nyingine tuambieni ila kama ni amani hii tuijuayo mnapotoka kwani amani hiyo amabyo tunaitambua sote si kufanya vurugu za kuchoma magari kuvunja makanisa nk. Na kiukweli kwa kufanya hivyo mnaidhalilisha dini ya amani dini ya kiislamu kwa hiyo mlioyafanya sio amani ni vurugu na katika dini ya kislamu achili mabili kikiristo si sawa.
Kutokana na hayo mnataka kuniambia kuwa waislamu ndio wanao onewa kuliko watu wote duniani? Na je? wao ndio wnahasira kuliko mtu yeyote hapa duniani? Angalie kwa makini mambo hayo na kisha tafakarini tena na tena je maandamano yale vurugu zile za kuvunga barabara na kuchoma magari na makanisa na chukulia pia kisa kizima cha mtoto wa miaka 14 kukojolea msahafu je lile ndilo lilikuwa suluhisho? kama jibu lako ni ndio itakuwa sio mzima wewe pia. Wote mtakua ndio walewale wenye maamuzi ya kukurupuka na mwisho wa siku haisaidii chochote. Wito wangu kwa watanzania wote wapenda amani kumbukeni sheria ipo na inauwezo wa kuwa suluhisho la matatizo yetu wote iwapo tu wote tutakuwa kitu kimoja kuhakikisha sheria haipindishi kwa ajili ya manufaa ya watu wachache. Natambua waislamu mlikuwa na uwezo wa kusimamia suala hili kisheria na haki ingetendeka. Zaidi nilihuzunika sana kuona mpaka wazee ambao wanaonekana wnahekima na busara wakiwa ni miongoni mwa wavunja makanisa na kuchoma magari wakati wao walistahili kuwasihi vijana na watoto wawe watulivu ilis sheria ifauate mkondo laki ilikuwa ni sifuri kiakiri maalifa na hekima sikuona mtoto nani kijana nani na mzee nani wote walikuwa sawa tu kwa kisa kimoja cha mtoto kukojolea msahafu.
Ninayo mengi sana ya kuongea laki hayo machache sana naomba yasielewe vibaya ni kujaribu kuwafumbua macho waliokuwa hawajui nini kilikuwa kinaendelea na pia kuwakumbusha waliosahau kuwa sheri ipo, lakini pia wale wanaopenda kuhukumu wakati MUNGU yupo kwa ajili ya kazi hiyo kwa yeye ndie aliyeumba na anahaki ya kumhukumu yeyote atakavyo. NB:- kila mtu anahasira jaribu kumudu hasira na nashangaa sana iweje wenye hasira wawe waislamu peke yao. Wale waoishi Tanga kama utaweza kukumbuka kisa cha shekhe wa msikiti mmoja jina ninalo ambae katika mwezi wa ramadhani tena siku ya ijumaa akiwa amefunga alitoa tamko katika spika kubwa na kusema muislamu naefanya mapenzi na mkristo au mpagani amefanya mapenzi ka kafiri kiliwauma wengi lakini hakuna alieandamana lakini MUNGU akaonyesha kuwa naweza mwezi huohuo wa ramadhani saa saba mcha shekhe yuleyule aliehtubia akafumaniwa na mke wa mtu gesti tena mwanamke huyo alikuwa mkristo. Najua wale wa tanga hasa barabara za namba nnakumbuka tukio hilo lakini pia matukio ya walimu wa mdrasa kulawiti watoto wakiume kama mnakumbuka iringa daresalam na Tanga matukio hayo yasharipotiwa na yanajulikana, kila binadamu hajakamilika hata Emanueli aliekojolea msahafu kama motto ambae hajakua kuakili hajakamilika sio malaika alipaswa apokewe hivyo kama wadhambi wengine ya hwa walawiti wazinzi tena wakiwa ni viongozi na walimu wa dini. Mwisho makala yangu fupi mahali ambapo nimekugusa ma nimekukosea naomba NISAMEHEWE BURE KUMBUKA MIMI PIA SIO MALAIKA NA SIKUA NA NIA MBAYA NI KUSEMA AMBACHO WATANZANIA WENGI WANAKIWAZA LAKINI WNASHINDWA KUKISEMA. NATUMAI MMENISAMEHE KWA MOYO MKUNJUFU. AMEN.
4 comments:
Appreciate this post. Let me try it out.
Feel free to surf to my web-site - dating online, bestdatingsitesnow.com,
Good article! We are linking to this great post on our website.
Keep up the great writing.
Look into my website WeldonTRause
Informative article, totally what I wanted to find.
Also visit my web-site; EugenioPStechlinski
Hello just wanted to give you a quick heads up. The text in your content seem to be running off the screen in Safari.
I'm not sure if this is a formatting issue or something
to do with browser compatibility but I figured I'd post to let
you know. The layout look great though! Hope you get the problem solved
soon. Kudos
Check out my blog SilvanaUUchiyama
Post a Comment