|
Cage maalum ya kukuzia vifaranga wachache.. |
|
Sehem maalu imezungushiwa wigo kwa ajili ya kulea vifaranga kwa kutumia taa za umeme. |
|
Sehemu unayoweza kulea vifaranga kwa maeneo ya wazi na maeneo ya Baridi na hata kuku wakubwa unaweza kuwalea katika nyumba kama hii. |
|
Hii ni nyumba ya wafanyabiashara wakubwa ama makampuni yanayojishughulisha na uleaji vifaranga.. |
Utangulizi
Kwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa kuku mwenyewe. Hivyo
ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige kuku anavyofanya. Ikumbukwe kuwa vifaranga
husumbuliwa zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa
na kukosa uangalizi wa karibu.
Ni lazima vifaranga waangaliwe kwa kuwapatia nyumba yenye joto, chakula kinachofaa
na maji safi , kuwakinga dhidi ya magonjwa masumbufu kwenye eneo husika na kuwatibu
wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri ambao
hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida.