Translate this blog in your favourable language

Saturday, January 11, 2014

IJUE NYUMBA YA KULELEA VIFARANGA WA SIKU 1 HADI WIKI 4 KITAALAM [MWONGOZO KWA MFUGAJI WA KUKU]

Cage maalum ya kukuzia vifaranga wachache..

Sehem maalu imezungushiwa wigo kwa ajili ya kulea vifaranga kwa kutumia taa za umeme.
Sehemu unayoweza kulea vifaranga kwa maeneo ya wazi na maeneo ya Baridi na hata kuku wakubwa unaweza kuwalea katika nyumba kama hii.

Hii ni nyumba ya wafanyabiashara wakubwa ama makampuni yanayojishughulisha na uleaji vifaranga..

Utangulizi

      Kwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa kuku mwenyewe. Hivyo
ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige kuku anavyofanya. Ikumbukwe kuwa vifaranga
husumbuliwa zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa
na kukosa uangalizi wa karibu.
     Ni lazima vifaranga waangaliwe kwa kuwapatia nyumba yenye joto, chakula kinachofaa
na maji safi , kuwakinga dhidi ya magonjwa masumbufu kwenye eneo husika na kuwatibu
wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri ambao
hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida.
Wafugaji wengi vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga vifaranga wake kwa muda
mrefu hadi wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku kurudia kutaga na hivyo kupata
vifaranga wachache zaidi kwa mwaka. Lakini vifaranga vikiondolewa kwa kuku mapema,
kama majuma matano hivi baada ya kuanguliwa, na wakatunzwa na mfugaji, kuku hutaga
mapema na idadi ya kuku kwa mfugaji huongezeka haraka ndani ya kipindi kifupi.
Mwongozo huu unaeleza jinsi ya kufuga vifaranga vizuri ili hatimaye mfugaji apate faida
zaidi.

Nyumba ya kulelea Vifaranga

Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufi kirie yafuatayo:-
a Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua
vifaranga wako mara kwa mara.
b) Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo
ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.
c) Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia.
Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.
d) Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta
chakula na maji bila kubanana.
e) Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku
wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa
na upepo.
Ukubwa wa Nyumba
Eneo: Vifaranga hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi
inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba
yenye meta 10 za mraba inatosha kulea vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo
vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa
3.25. Utajenga kutegemea na eneo ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na
uwape vifaranga eneo la kuwatosha.
Sakafu: Sakafu nzuri katika nyumba ya vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti
iliochanganywa na zege. Ili kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi
vinavyopatikana kirahisi katika eneo lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa
kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la
sakafu.
Ukuta: Ingefaa kuta za nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe.
Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu ili kurahisisha usafi shaji wa nyumba au umwagiaji
wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta
0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye
meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fi to.
Mbao: Nguzo za miti au mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu
ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea
na wadudu.
Madirisha: Unaweza kutumia maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na
yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe
misumari kwenye ubao ili ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na
mwanga wa kutosha katika nyumba ya vifaranga.
Paa: Mjengo wa paa uwe unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na
tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe,
mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja
iezekwe bila kuchelewa.

Vyombo kwenye nyumba ya vifaranga

Kuna vyombo vingi pia njia nyingi zinazotumika katika kulea vifaranga kutegemeana na hali
halisi ya mfugaji. Mfugaji kijijini anaweza kutumia vyombo vifuatavyo:
1. Vitalu
Vifaranga hutunzwa ndani ya kitalu
kilichotengenezwa kwa mbao au karatasi
ngumu zinazotumika kujengea dari.
Au katika mazingira ya kijijini unaweza
kutengeneza wigo wa mduara kwa
magunia. Upana wake uwiane na wingi wa
vifaranga ulionao na kina chake kama mita
moja. Ukuta wake uwe na tabaka mbili za
magunia hayo zilizoachana kwa nafasi
ya inchi tatu au nne. Katikati ya nafasi
hiyo jaza maranda ya mbao au pumba za
mpunga. Tayari utakuwa umepata kitalu
cha kulelea vifaranga.
Ndani ya kitalu weka taa ya chemli ya kutoa joto linalohitajika kwa vifaranga.
2. Taa ya chemli (taa ya mkono)
Kutegemeana na hali ya hewa taa moja ya chemli inaweza kulea vifaranga 50 au zaidi.
Hakikisha kuwa unayo akiba ya mafuta ya taa ya kutosha, vioo, utambi n.k. Taa moja
hutumia debe moja la mafuta ya taa kwa muda wa siku 16 hadi 20. Unashauriwa uweke
mafuta kwenye taa asubuhi na kukagua jioni kama yanatosha kwa sababu taa ikizimika
usiku utapata hasara ya vifo kwa vifaranga kujikusanya na kukosa hewa .Weka mafuta ya
kutosha lakini usijaze taa. Joto la taa za chemli hurekebisha kwa kupandisha au kushusha
utambi pia kuongeza au kupunguza idadi ya taa.
3. Jiko la Mkaa
Jiko la mkaa linaweza kutumika badala ya taa kwa ajili ya kuwapa vifaranga joto. Unapotumia
jiko la mkaa ni hakikisha kwamba mkaa unaotumia hautoi moshi na chumba kinapitisha
hewa safi na ya kutosha. Pia jiko liwekwe juu ya matofaili ili kuzuia vifaranga wasiliguse.
4. Mwamvuli
Mfugaji akimudu anaweza kutengeneza mwamvuli wa kuning’inia juu ya kitalu cha kulea
vifaranga kwa kutumia makaratasi magumu ya “hardboard”. Mwamvuli unasaidia kupunguza
upotevu wa joto na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya taa. Kwenye mwamvuli wa
duara toboa tundu moja ili kupitisha hewa yenye joto. Angalia mviringo wa mwamvuli wako
uwiane na ukubwa wa kitalu chako. Ili kuwapa vifaranga uhuru wa kufuata au kuepuka joto.
Ni lazima mwamvuli uwekwe juu ya matofali na kila juma inabidi uinuliwe juu kiasi cha cm 5
(inchi 2, kufuatana na hali ya hewa.
5. Vyombo vya chakula (Vihori)
Ili vifaranga wakue vizuri vyombo vya
chakula lazima viwafae. Vipimo pamoja na
idadi ya vyombo vya chakula ni vya muhimu
viwatosheleze. Chombo chenye urefu wa (futi
3 x inch 3) kinatosha vifaranga 100. Ukitumia
mbao kutengeneza vyombo vya chakula
unashauriwa mbao ziwe unene wa cm 1/25
(inchi ½). Pia, unaweza kutumia sahani za
kawaida unazotumia nyumbani kuwawekea
vifaranga chakula.
Chombo cha kulishia vifaranga
6. Vyombo vya maji:
Chombo chochote chenye kina kifupi kinafaa kwa
kuwayweshea kuku ila budi kiinuliwe ili vifaranga wasiweze
kuingiza takataka za chini kwenye maji. Pia kama ni cha wazi
maji yawekewe changarawe safi kabisa ili kuzuia vifaranga
wasiloane maji. Au tumia sahani na makopokama ifuatavyo.
Toboa sentimita tatu kutoka kwenye mdomo wa kopo, jaza
maji katika kopo halafu lifunike kwa sahani na ligeuze.
Kinywesheo cha vifaranga

   Itaendelea... Mawasiliano ya mtaalam 0753226438 kwa msaada zaidi.

Post a Comment

Google+ Badge