Mara nyingi sana kuku mgojwa huwa namna hii,, |
Ugonjwa
ni nini? Ugonjwa ni mabadiliko kutoka katika afya ya kawaida ya
mnyama/kuku. Hali hii hutokea pale
vimelea au vijidudu
vinapoingia mwili wa mnyama, kwa kula vyakula vyenye sumu, au inapotokea kuna
uhaba wa lishe au madini mwilini.
TOFAUTI
ZA MUONEKANO KATI YA KUKU MWENYE AFYA NA KUKU MGONJWA
Ø Macho
na sura angavu
Ø Hupenda
kula na kunywa maji
Ø Pua
zilizo safi, upanga na undu mwekundu, manyoya
laini na yaliyopangika vizuri
Ø Hupumua
kwa utulivu
Ø Sehemu
ya kutolea haja huwa kavu
Ø Kinyesi
kikavu, cheupe na kisicho na rangi
Ø Hutaga
mayai kawaida
KUKU ASIYE NA AFYA NZURI
Ø Hula
na kunywa kidogo au zaidi ya kawaida
Ø Hutoa
kamasi puani, ute na matongotongo; manyoya
yaliyovurugika
Ø Hupumua
kwa shida na kwa sauti
Ø Sehemu
ya kutolea haja inakuwa na unyevunyevu na
kinyesi kuganda
Ø Huharisha,
kinyesi huwa na damu au minyoo
Ø Hutaga
mayai machache au husimama kutaga kabisa
Ø Huwa
na tabia ya kujitenga na wenzake katika kundi
MGONJWA MUHIMU
YANAYOSABABISHWA NA BACTERIA
HOMA
KALI YA MATUMBO (FOWL TYPHOID)
Maelezo: Ni ugonjwa wa kuku
unaosababishwa na bacteria na hushambulia zaidi kuku
Wakubwa pia na
vifaranga. Ugonjwa pia hushambulia aina zote za bata, kanga na ndege
wa porini.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea: Chanzo
cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa
na kinyesi cha kuku
wagonjwa. Panya, ndege na wanyama wengine wanaweza kueneza
ugonjwa kwa kubeba
mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa na kuchafua maji na vyakula.
Maambukizi pia
yanaweza kupitia katika mayai yanayototolewa na vifaranga kuathirika. Pia
mashine za kutotolea zilizochafuliwa zinaweza kuambukiza vifaranga.
Dalili
Kuku
wakubwa
Ø Kuharisha
kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano
Ø Vifo
vya ghafla
Ø Kupauka
kwa upanga na masikio kwa sababu ya kupungukiwa damu
Ø Manyoya
hutimka, hushusha mbawa, hufumba macho na kuzubaa (kuvaa koti)
Vifaranga
Ø Vifaranga
wanatotolewa wakiwa wamekufa au dhaifu
Ø Hujikusanya
pamoja na kukosa hamu ya kula
Ø Kinyesi
cha rangi ya njano na huganda kwenye manyoya ya sehemu ya kutolea haja
Ø Hupumua
kwa haraka na kwa shida
Ø Vifo
vingi huweza kutokea kuku wasipotibiwa
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø Kinyesi
cha rangi ya njano na kijani kwenye manyoya ya sehemu ya kutolea haja kubwa
Ø Misuli
iliyovia na damu kuwa nyeusi
Ø Ini
lililovimba na kuwa na rangi ya pinki
Ø Bandama
lililovimba
Ø Figo
na mayai yaliyovia
Ø Mabaka
meupe kwenye sehemu ya juu ya figo
Tiba
v Yapo madawa
mengi aina ya antibiotiki ambayo yanaweza kupunguza vifo vinavyotokana
na ugonjwa.
Lakini madawa haya hayawezi
kumaliza kabisa ugonjwa kutoka shambani.
v Pata ushauri wa
daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø Hakikisha
kwamba vifaranga wako wanatoka katika mashamba ambayo hayana huu ugonjwa
Ø Panga
utaratibu wa kuchunguza afya za kuku wako mara kwa mara na kuondoa/kuchinja
kuku
wanaonyesha dalili za
ugonjwa.
Ø Weka
utaratibu wa kuhakikisha watu, wanyama, ndege wa aina nyingine na ndege wa
porini hawazururi
shambani.
Ø Fanya usafi wa mabanda na mazingira
mara kwa mara unapobadilisha makundi ya kuku kwa kutumia
viuatilifu
vilivyopendekezwa.
Aina nyingine ya Homa
ya Matumbo (Avian Paratyphoid) inafanana na aina iliyoelezwa hapo juu,
tofauti kubwa
ni aina ya vimelea
vinavyosababisha aina hii ya homa, na huathiri zaidi kuku na bata wadogo.
HOMA
YA MATUMBO (AVIAN PARATYPHOID)
Maelezo:
Ni ugonjwa wa kuku unaosababishwa na bakteria wa spishi tofauti na
ya bakteria wanaosababisha homa
kali ya matumbo na
hushambulia zaidi kuku na bata wadogo. Vimelea vya ugonjwa huu huweza
kusababisha homa ya matumbo kwenye binadamu.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø Chanzo cha maambukizi ni maji na
chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa. Panya, mbwa,
Ø ndege
na wanyama wengine wanaweza kueneza ugonjwa kwa kubeba mizoga ya kuku waliokufa
kwa
Ø ugonjwa
na kuchafua vyanzo vya maji na vyakula.
Ø Maambukizi
pia yanaweza kupitia katika mayai yanayototolewa na vifaranga kuathirika. Pia
mashine za kutotolea zilizochafuliwa zinaweza kuambukiza vifaranga.
Dalili
Vifaranga
Ø Vifaranga
wanatotolewa wakiwa wamekufa au mara tu baada ya kuanguliwa
Ø Hujikusanya
pamoja karibu na joto
Ø Uharo
kuganda kwenye manyoya ya sehemu ya kutolea haja
Ø Vifo
kwenye vifaranga vinaweza kufikia hadi asilimia 50.
Kuku wakubwa
Ø Vifo
vya ghafla Kuharisha kinyesi cha majimaji na cha rangi ya njano
Ø Kuku
kuharisha
Ø Kupungua
kwa uzito
Ø Kuku
wa mayai hupunguza utagaji
Ø Kuku
anaonekana mchovu
Uchunguzi wa
Mzoga
Mabadiliko muhimu
katika mzoga wa kifaranga ni:
Ø
Ini kuvimba na kuvia
Ø
Uvimbe mweupe mdogo mdogo kwenye ini
Ø
Mapafu kuvia
Ø
Utumbo kuvimba
Ø
Njano ya yai kutapakaa tumboni
Tiba
Ø Yapo madawa
mengi aina ya antibiotiki na sulfa ambayo yanaweza kupunguza vifo
vinavyotokana na
ugonjwa. Lakini madawa haya
hayawezi kumaliza kabisa ugonjwa kutoka shambani.
Ø Pata ushauri wa
daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø
Hakikisha kwamba vifaranga wako wanatoka katika mashamba ambayo
hayana huu ugonjwa.
Ø
Panga utaratibu wa kuchunguza afya za kuku wako mara kwa mara na
kuondoa/kuchinja kuku
wanaonyesha dalili za
ugonjwa.
Ø
Weka utaratibu wa kuhakikisha watu, wanyama, ndege wa aina
nyingine na ndege wa porini hawazururi
shambani.
Ø
Fanya usafi wa mabanda na mazingira mara kwa mara unapobadilisha
makundi ya kuku kwa kutumia
viuatilifu
vilivyopendekezwa.
Ø Mayai
yakusanywe mara kwa mara
Ø Hakikisha
vifaranga wanapata joto la kutosha.
KUHARISHA
KINYESI CHEUPE (BACILLARY WHITE DIARRHEA)
Maelezo
Ni ugonjwa wa kuku
unaosababishwa na bakteria na hushambulia zaidi kuku wadogo wenye umri hadi
wiki tatu. Ugonjwa pia hushambulia aina zote za bata, kanga na ndege wa porini
(mbuni).
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø
Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na
kinyesi cha kuku wagonjwa. Panya, ndege na wanyama wengine wanaweza kueneza
ugonjwa kwa kubeba mizoga ya kuku iliyokufa kwa ugonjwa na kuchafua maji na
vyakula.
Ø
Kuku waliopona baada ya matibabu wanaweza kuendelea kuchafua
mazingira na kuwa chanzo cha
maambukizi, hivyo
waondolewe shambani.
Ø
Maambukizi pia yanaweza kupitia katika mayai yanayototolewa na
vifaranga kuathirika.
Tahadhari: Wageni na
wafanyakazi wanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba hadi shamba au
banda hadi banda.
Ø
Vituo vya kutotolea vifaranga vinaweza kuwa chanzo. Hakikisha
vifaranga wako hawatoki kwenye kituo chenye kuku wagonjwa.
Dalili
Vifaranga
Ø
Vifo vya ghafla
Ø
Vifaranga wanatotolewa wakiwa wamekufa au dhaifu
Ø
Hujikusanya pamoja karibu na taa kwa ajili ya kupata joto
Ø
Uharo wa rangi nyeupe kama chaki
Ø
Hupumua kwa shida
Ø
Uharo huganda kwenye manyoya ya sehemu ya kutolea haja
Ø
Vifaranga wanapiga sana kelele
Ø
Vifaranga wanaonyesha ulemavu
Ø
Kuvimba magoti
Kuku
wakubwa
Ø
Kuku wakubwa huonyesha dalili za ugonjwa sugu
Ø
Kupauka kwa upanga na masikio kwa sababu ya kupungukiwa damu
Ø
Utagaji wa mayai hupungua
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø
Njano ya yai iliyotapakaa tumboni mwa kuku
Ø
Uvimbe mdogo mdogo wa rangi ya kijivu ulioenea kwenye
moyo,firigisi, misuli, mapafu na sehemu ya nje ya utumbo katika kuku wakubwa
(umri wa wiki 2 hadi 5)
Tiba
Ø Yapo madawa
mengi aina ya antibiotiki ambayo yanaweza kupunguza vifo vinavyotokana
na ugonjwa.
Ø Lakini madawa
haya hayawezi kumaliza ugonjwa shambani kabisa.
Ø Pata ushauri wa
daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø
Hakikisha kwamba vifaranga wako wanatoka katika vyanzo
vilivyothibitishwa kuwa havina huu ugonjwa
Ø
Tengeneza utaratibu wa kufanya usafi wa mabanda na mazingira mara
kwa mara unapobadilisha makundi
ya kuku kwa kutumia
viuatilifu vilivyopendekezwa.
Ø Panga
utaratibu wa kuchunguza afya za kuku wote wenye umri zaidi ya miezi mitano (5)
mpaka hapo
kundi lote
litakapoonyesha kwamba hakuna kuku mwenye maambukizi, kuku salama wahamishiwe
katika mabanda safi.
Ø Weka
utaratibu wa kuhakikisha watu, wanyama, ndege wa aina nyingine na ndege wa
porini hawazururi
shambani au bandani.
KIPINDUPINDU
CHA KUKU (FOWL CHOLERA)
MAELEZO
Ni ugonjwa wa kuku unaosababishwa na
bacteria ambao huenea kwa haraka na kusababisha vifo vingi. Ugonjwa hushambulia
kuku na ndege wa aina zote ijapokuwa jamii ya bata huathirika zaidi kuliko
kuku.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø Chanzo
cha maambukizi ni hewa, maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku
wagonjwa.
Ø Kwa
kawaida ugonjwa huanza kwa kuingiza katika shamba/banda kuku wagonjwa kutoka
nje. Baada ya
vimelea kuingia
huenea kwa kupitia maji au vyakula vilivyochafuliwa.
Ø
Udongo uliochafuliwa na kinyesi cha kuku mgonjwa huweza kuchafua
maji na vyakula
Ø
Hewa kutoka kwa kuku wagonjwa inaweza kuwa chanzo cha maambukizi.
Ø
Panya, ndege na wanyama wengine wanaweza kueneza ugonjwa kwa
kubeba mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa na kuchafua maji na vyakula.
Dalili
Kuku wanaweza
wasionyeshe dalili zozote za ugonjwa, lakini dalili zifuatazo zinaweza
kuonekana:
Ø
Vifo vya ghafla vya idadi kubwa ya kuku waliokuwa na afya
Ø
Kuku wanakonda
Ø
Kuku wanapumua kwa shida, wanakohoa na kupiga chafya
Ø
Uharo wa rangi ya kijivu, njano au kijani na unaonuka
Ø
Vifaranga wanaonyesha ulemavu
Ø
Kuvimba magoti na kifundo cha mbawa
Ø
Kichwa, upanga na undu hugeuka kuwa rangi nyeusi au zambarau
Ø
Vifo vya kuku vinaweza kufikia asilimia 20
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø
Madoa ya damu kwenye mapafu, utumbo na kuzunguka moyo.
Ø
Ini huvimba, laini na kuonekana kama limepikwa.
Ø
Uchafu mgumu uliogandamana katika eneo linalozunguka utumbo,
kwenye masikio na machoni
Ø
Pua na mdomo kuwa na makamasi mazito na machafu
Tiba
v Yapo madawa
mengi aina ya antibiotiki na sulfa ambayo yanaweza kutumika kwa
ajili ya tiba na kinga.
v Pata ushauri wa daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø Utaratibu
ulio mzuri zaidi ni kuondoa kuku wote kutoka kwenye shamba/banda ambalo ugonjwa
umethibitishwa,
kupuliza dawa za viuatilifu kabla ya kuingiza vifaranga na kuku wapya
Ø Mabanda
yote ya kuku yapuliziwe dawa za viuatilifu kabla ya kuingiza kuku wapya.
Kuku wapya
watenganishwe na kuchunguzwa kwa muda wa angalau mwezi mmoja kabla ya
kuwachanganya na kuku
wengine.
Ø Vifaranga
visichanganywe na kuku wakubwa.
Ø Hakikisha
unafuata kanuni za ufugaji bora ili kuku wakue vizuri na wasiathirike
MAFUA YA KUKU (INFECTIOUS CORYZA )
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria ambao
hushambulia zaidi kuku na ndege wa porini. Ugonjwa
hushambulia kuku wa
umri wowote.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø
Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na
kinyesi cha kuku wagonjwa.
Ø
Kuku au ndege wagonjwa huambukiza wenzao kupitia mfumo wa hewa
wanapopiga chafya.
Dalili
Ugonjwa huu
hushambulia zaidi mfumo wa hewa na hivyo kusababisha dalili zifuatazo:
Ø
Makamasi mazito yenye usaha hutoka puani
Ø
Kuku anashindwa kupumua, hukohoa na kupiga chafya
Ø
Harufu mbaya kutoka kinywani na machoni
Ø
Uso mzima unavimba pamoja na upanga
Ø
Vifo vya kuku vinaweza kufikia asilimia 20
Tiba
Ø Madawa aina ya sulfa
na antibiotiki yanaweza kutumika kwa ajili ya tiba na kinga.
Ø Pata ushauri wa
daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø Iwapo
ndani ya shamba moja kuna kuku wa aina tofauti, k.m. vifaranga, kuku wazazi,
kuku wakubwa,
jaribu kuwatenganisha
ili mabanda yao yasikaribiane
Ø Pale
inapowezekana, jaribu kupanga utaratibu wa kila kundi la kuku lishughulikiwe na
mfanyakazi wake ili kuzuia kueneza maambukizi.
Ø Hakikisha
kuku wagonjwa wanatengwa na wale wazima
Ø Tumia
maji yaliyowekwa dawa aina ya klorini
Ø Weka
utaratibu wa kuhakikisha watu, wanyama, ndege wa aina nyingine na ndege wa
porini hawazururi
shambani.
UGONJWA SUGU WA MFUMO WA HEWA
(CHRONIC RESPIRATORY DISEASE-CRD)
MAELEZO
Ni ugonjwa
unaosababishwa na bakteria ambao hushambulia zaidi kuku na bata mzinga.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø
Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na
kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye
Vimelea. Pia kupitia
mfumo wa hewa kutoka ndege wagonjwa.
Ø
Njia kuu ya kuenea kwa maambukizi ni kupitia mayai, hivyo
maambukizi huendelea kutoka kizazi hadi
Kizazi.
Ø
Tahadhari: Wageni, wafanyakazi na magari yanaweza kusambaza
ugonjwa kutoka shamba hadi shamba au banda hadi banda
Dalili
Ugonjwa huu
hushambulia zaidi mfumo wa hewa na hivyo kusababisha dalili zifuatazo:
Ø
Kuku hukoroma
Ø
Kuku hutoa makamasi
Ø
Kuku wanakohoa kwa muda mrefu, wiki hadi miezi
Ø
Kuvimba macho
Ø Kutingisha
kichwa
Ø Vifo
vya kuku vinaweza kufikia hadi asilimia 20
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø
Athari kubwa za ugonjwa huu ni kwenye mfumo wa hewa, hivyo
mabadiliko yanakuwa katika mfumo
mzima wa hewa.
Ø
Kamasi nzito zenye usaha zilizotapakaa kwenye pua, koromeo, mapafu
na vifuko vya hewa
Tiba
Ø
Madawa
aina ya sulfa na antibiotiki yanaweza kutumika kwa ajili ya tiba
na kinga.
Ø
Pata
ushauri wa daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø Weka
utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi na watu wengine wanazuiwa kuranda randa
kutoka banda
hadi banda. Ikiwa
lazima kufanya hivyo, basi pawepo utaratibu wa kuoga na kubadilisha nguo kati
ya
banda moja kwenda
jingine.
Ø Epuka
kuingiza kuku wagonjwa katika shamba/banda ambalo halina ugonjwa
Ø Hakikisha
mabanda yana joto linalostahili na mzunguko wa hewa mzuri, pia kuku wapewe
chakula cha Kutosha
KOLIBASILOSI
(COLIBACILLOSIS)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria na
hushambulia zaidi kuku na bata. Ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø Chanzo
cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku
wagonjwa. Bakteria
Wanaosababisha
ugonjwa wameenea kila mahali hivyo kuweza kuchafua maji na chakula.
Ø Vifaranga
wanaweza kupata maambukizi wakiwa bado ndani ya yai kabla ya kuanguliwa.
Ø Mayai
machafu yenye bacteria ndiyo njia kuu ya kuambukiza vifaranga kupitia kitovu
baada ya
kutotolewa. Pia mayai
yenye maganda dhaifu na makasha machafu ya kubebea mayai ni chanzo kingine
cha maambukizi.
Dalili
Ø
Kuku wanaonekana kuzubaa
Ø
Kuku wanatoa sauti ya chini chini
Ø
Kuku wanajikusanya karibu na taa inayotoa joto
Ø
Kuharisha na kinyesi kugandana katika njia ya haja
Ø
Ngozi ya kifuani ina uvimbe
Ø
Vifo vya vifaranga vinaweza kufikia asilimia 10, vifaranga walio
totolewa inaweza kufika asilimia 50.
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø Sehemu
ya haja inaweza kuzibwa na kinyesi kilichokauka
Ø Njano
ya yai kutapakaa tumboni, uchafu wenye rangi nyeupe au kijani, ukiwa na damu
Uvimbe kwenye ini, utumbo na utandu wa tumboni
Tiba
Ø Madawa aina ya sulfa
na antibiotiki yanayofaa yanaweza kutumika kwa ajili ya tiba na
kinga.
Ø Pata ushauri wa
daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø Angamiza
kwa kuchoma moto vifaranga wote ambao hawakui vizuri na wanaonyesha dalili za
ugonjwa
Ø Mabanda
yote ya kuku yapuliziwe dawa za viuatilifu kabla ya kuingiza kuku na vifaranga
wapya.
MAGONJWA MUHIMU YA
VIRUSI
Mdondo/Kideri,
Gumboro, Mareksi, Ndui ya Kuku, Mafua Makali ya Ndege na Ugonjwa
Unaoathiri Mfumo wa Fahamu.
MDONDO/KIDERI
(NEWCASTLE DISEASE)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao
hushambulia aina zote za spishi za ndege, ijapokuwa kuku ndio aina
inayoathirika zaidi. Binadamu na wanyama wengine pia wanaweza kuambukizwa.
Ugonjwa huathiri mifumo ya fahamu, njia ya chakula na hewa.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø
Chanzo cha maambukizi ni maji, chakula kilichochafuliwa na kinyesi
cha kuku wagonjwa. Pia maambukuzi huweza kupitia mfumo wa hewa kutoka kwa kuku
wagonjwa.
Ø
Kuku, vifaa vya kazi na bidhaa zitokanazo na kuku (nyama, mayai,
manyoya na mbolea) kutoka mashamba yenye ugonjwa zinaweza kueneza ugonjwa
kutoka shamba moja hadi jingine.
Ø
Vifaranga wanaweza kupata maambukizi kutoka vituo vya kutotolea
vifaranga kutokana na maganda ya
mayai
yaliyochafuliwa.
Dalili
Ø
Vifo vya ghafla vya idadi kubwa ya kuku katika shamba/banda
Ø
Kuku wanatetemeka na kushindwa kutembea
Ø
Kuku hupooza miguu, mabawa na kupinda shingo; na hujizungusha
mahali alipo
Ø
Kuku huharisha kinyesi cha kijani na wakati mwingine chenye
mchanganyiko wa rangi ya njano
Ø
Kuku huzubaa na kuacha kula
Ø
Kuku hukohoa, hupiga chafya na kupumua kwa shida
Ø
Vifo vinaweza kufikia asilimia
100, kutegemea na umri na aina ya ndege
Uchunguzi wa
Mzoga
Ugonjwa huathiri
zaidi mfumo wa hewa na njia ya chakula, hivyo mabadiliko yanayoonekana kwenye
mzoga ni pamoja na:
Ø
Madoa ya damu kwenye mfumo wa hewa
Ø
Kamasi nzito zenye rangi ya njano kwenye koromeo
Ø
Utandu mweupe kwenye mifuko ya hewa
Ø
Bandama kuvimba
Ø
Uvimbe kwenye kichwa na eneo la shingo
Ø
Madoa madogo madogo ya damu kwenye kifua, mafuta na utandu wa
tumboni
Ø
Damu kuvia kwenye mfumo wa usagaji chakula - juju, firigisi, tumbo
na utumbo
Tiba
Ø Hakuna tiba ya
ugonjwa huu ila kuku wapewe antibiotiki.
Ø Pata ushauri wa
daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø Weka
utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi , wageni na ndege hawaingii hovyo kwenye
shamba/banda
Ø Angamiza
mizoga yote kwa njia stahiki kwa kuchoma moto au kufukia kwenye shimo refu
ardhini.
Ø Hakikisha
banda la kuku lina hewa ya kutosha na epuka msongamano mkubwa wa kuku.
Ø Fanya
usafi wa mara kwa mara kwenye vyombo vya kuwekea maji na chakula, pamoja na
mabanda ya kuku.
Ø Zuia
uingizaji holela wa kuku wageni wasiochanjwa kwenye shamba/banda. Kuku
wanaoingia shambani/ bandani watoke maeneo yasiyokuwa na ugonjwa.
Ø Tenganisha
kuku kufuatana na umri
Ø Maeneo
yenye ugonjwa yawekwe chini ya karantini na mabanda yapulizwe dawa
Ø Kuku
wapewe Chanjo tangu vifaranga wa umri wa siku 3, baada ya wiki 3 – 4, na baadaye
kila baada ya miezi 3.
Gumboro
(Infectious Bursar Disease)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao
hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku na bata wadogo hadi wiki
12 ndio wanaoathirika zaidi.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø Chanzo
cha maambukizi ni maji, chakula na vifaa/vyombo vya shambani vilivyochafuliwa
na kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye vimelea.
Ø Maambukizi
pia huenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda.
Chukua Tahadhari: Wageni, wafanyakazi na
magari yanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba
hadi shamba au banda
hadi banda. Hii ni pamoja na kuku hai, vifaa/vyombo vya shambani na bidhaa
zitokanazo na kuku
(mayai, nyama, manyoya na mbolea) wanaosafirishwa kutoka mashamba/mabanda
yenye ugonjwa.
Dalili
Ø
Uharo mweupe wenye maji maji
Ø
Kuku wanadonoana kwenye sehemu ya kupitishia haja, na sehemu hii
huvimba
Ø
Kuku hulala kifudifudi
Ø
Kuku wanashindwa kutembea na wanatetemeka
Ø
Vifo vya kuku vinaweza kufikia hadi asilimia 30, na kupungua jinsi
wanavyozeeka
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø
Sudi (mkia) ya kuku huvimba mara mbili ya kawaida na kujaa maji.
Ø
Madoa ya damu kwenye miguu na mapaja.
Tiba
Ø
Hakuna
tiba maalum
Ø
Kuku
wapewe vitamini na maji kwa wingi
Ø
Antibiotiki husaidia maambukizi nyemelezi.
Ø
Pata
ushauri wa daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø
Mizoga, makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa
vichomwe moto au kuzikwa.
Ø
Weka utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa
Ø
Baada ya kumaliza kuwauza kuku wote, fanya usafi wa mabanda na
kupuliza dawa
Ø
Weka utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi , wageni na ndege
hawaingii hovyo kwenye shamba/banda
Ø
Kuku wapatiwe Chanjo katika
maji ya kunywa (angalia Ratiba)
MAREKSI
(MAREK’S DISEASE)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao
hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku wa mayai ndio
wanaoathirika zaidi. Mara nyingi ugonjwa hutokea katika kuku wenye umri kati ya
wiki 12 hadi 24, ijapokuwa hata kuku wakubwa nao hupata ugonjwa.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø Maambukizi
pia kuenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda na
vumbi
litokanalo na
manyoya.
Ø Mate
ya kuku wagonjwa pia ni njia mojawapo ya maambukizi
Ø Binadamu,
inzi na aina nyingine za ndege pia zinaweza kusambaza maambukizi.
Dalili
Ø
Uharo mweupe wenye maji maji
Ø
Mboni ya jicho kuwa na rangi ya kijivu
Ø
Upofu kwenye kuku
Ø
Miguu na mabawa hupooza
Ø
Kuku kupindisha kichwa
Ø
Kwa kawaida vifo ni kati ya asilimia 10 na 80.
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø
Uvimbe
mweupe karibu katika viungo vyote laini vya mwili: maini, figo, bandama na
ngozi.
Ø
Mishipa
ya fahamu kuvimba katika miguu na mbawa zilizopooza
Tiba
Ø Hakuna tiba
maalum
Ø Pata ushauri wa
daktari
Kuzuia na Kinga
Ø Mizoga,
makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa vichomwe moto au
kuzikwa.
Ø Weka
utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa
Ø Baada
ya kumaliza kuwauza kuku wote, fanya usafi wa mabanda na kupuliza dawa
Ø Hakikisha
unatenganisha kuku wadogo na wakubwa hadi miezi 3, na watenganishe kuku kwa
umri
Ø Vifaranga
vya siku moja vipatiwe Chanjo dhidi ya ugonjwa (angalia
Ratiba)
NDUI
YA KUKU (FOWL POX)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambavyo
hushambulia zaidi kuku, jamii ya bata na aina nyingi ya ndege pori. Kuku na
ndege wa umri tofauti wote huweza kushambuliwa na sehemu zinazoathirika zaidi
ni zile zisizo na manyoya. Virusi vinaweza kuishi katika mazingira kwa muda
mrefu.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø
Chanzo cha maambukizi ni vifaa/vyombo vya shambani
vilivyochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye vimelea.
Ø
Maambukizi pia kuenea kupitia wadudu wanaouma kama chawa, kupe,
nzi weusi na mbu.
Ø
Maambukizi pia kuenea kupitia majeraha wanayoyapata kuku
wanapopigana na kukwaruzana au kugusana
Ø
Maambukizi kupitia mfumo wa hewa na chakula
Dalili
Ø Ugonjwa
unapoathiri ngozi hutokea vidutu vikubwa vya rangi ya kijivu au kahawia kwenye
upanga, undu, macho na mdomoni
Ø Ugonjwa
unapoathiri sehemu laini za mwili, mabaka
madogo meupe hutokea
kwenye kona za mdomo, kuzunguka ulimi, ndani ya mdomo na kwenye koo
Tiba
Ø Hakuna tiba
Ø Kuku wanaweza kupewa
vitamini na glucose kupunguza makali ya ugonjwa
Ø Antibiotiki na maji yenye
chumvi husaidia maambukizi nyemelezi.
Ø Pata ushauri wa
daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø Kuku
wote walioathirika waondolewe shambani/bandani.
Ø Mizoga,
makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa vichomwe moto au
kuzikwa.
Ø Pulizia
kemikali za kuua wadudu
Ø Weka
utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa japokuwa
inawezekana visiuwe
virusi wote
Ø Kuku
wapatiwe Chanjo wakiwa na wiki 6. Maeneo mengine chanjo inatakiwa
kufanywa mapema zaidi. (Angalia Ratiba).
MAFUA
MAKALI YA NDEGE (HIGHLYPATHOGENIC AVIAN INFLUENZA )
Maelezo
Ni ugonjwa
unaosababishwa na virusi ambao hushambulia aina zote za ndege pamoja na
binadamu.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø Chanzo
cha maambukizi ni mayai yaliyoambukizwa, ndege wagonjwa na mashine za kutotolea
Ø Zilizochafuliwa
na kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye vimelea.
Ø Maambukizi
huenea kupitia maji maji ya kuku wagonjwa, kinyesi, vifaa na nguo za
wafanyakazi na maji ya kunywa.
Ø Mayai
yaliyoambukizwa yakipasuka katika mashine za kutotolea yanaweza kuambukiza
vifaranga na
Ø kufanana
na maambukizi yanayotoka kizazi kimoja hadi kingine
Dalili
Ø
Vifo vya ghafla
Ø
Kelele za kawaida za kuku hazisikiki tena
Ø
Kuku hukohoa
Ø
Pua kutoa makamasi na macho machozi
Ø
Kuvimba kwa uso
Ø
Upanga na undu zinakuwa na rangi ya bluu
Ø
Uharo (mara nyingi wa rangi ya kijani)
Ø
Dalili za kuathirika mfumo wa fahamu, kama vile kupooza
Ø
Kuku wengi huambukizwa lakini vifo ni vichache, asilimia 5 hadi
50.
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø
Uharo wenye damu.
Ø
Njia ya hewa kuvimba – pua, koromeo, mifuko ya hewa pamoja na
utandu wa macho
Ø
Ovari zinakuwa na madoa ya damu na kupungua ukubwa
Ø
Upanga na undu zinakuwa na rangi ya bluu
Ø
Kichwa na shingo kuvimba
Ø
Mzoga unaonekana umekauka
Ø
Misuli imevia
Ø
Madoa ya damu kwenye firigisi na mafindofindo ya tumboni
Tiba
Ø
Hakuna
tiba maalum
Ø
Pata
ushauri wa daktari
Kuzuia na Kinga
Ø Mizoga,
ndege wagonjwa, makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa
vichomwe moto
au kuzikwa.
Ø Weka
utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa kwenye mabanda na
vyombo
Ø Baada
ya kumaliza kuwauza kuku wote, fanya usafi wa mabanda na kupuliza dawa
Ø Weka
utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi , wageni na ndege kutoka kwa majirani
hawaingii ovyo
kwenye shamba/banda
Ø Kuku
wanaotoka nje ya shamba wawekwe kwenye karantini kabla ya kuingizwa
shambani/bandani
Ø Zuia
ndege wa porini wasiingie kwenye mabanda
MAGONJWA MUHIMU YA PROTOZOA
Maelezo
Protozo ni vimelea vyenye chembe moja ambavyo
husababisha magonjwa kwenye ndege na wanyama.
Mazingira ya joto na
unyenvuyevu husababisha kuongezeka kwa Protozoa. Maambukizi mengi ni kwa njia
ya kinyesi cha ndege wagonjwa kuchafua maji na chakula, nguo na viatu vya
wafanyakazi, pamoja na nzi na wadudu wengine. Magonjwa muhimu yanayosababishwa
na protozoa kwenye kuku nchini Tanzania ni: Kuhara Damu na Histomonasi.
KUHARA
DAMU (COCCIDIOSIS)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na Protozoa ambao
hushambulia kuku na wanyama wengine. Ugonjwa huathiri kuku wadogo na wakubwa.
Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
Ø Maambukizi
huenea kupitia kinyesi cha kuku wagonjwa kuchafua maji na chakula, udongo na
maranda.
Ø Njia
kuu ya maambukizi ni kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa na vimelea
Ø Maambukizi
yanaweza pia kupitia vifaa na vyombo vya shambani, nguo, wadudu na wanyama.
Dalili
Ø Kuhara
damu
Ø Mbawa
kushuka
Ø Kuzubaa
na kuacha kutaga
Ø Kukosa
hamu ya kula
Ø Kupunguza
kasi ya ukuaji na uzito
Ø Kwa
kawaida vifo ni vingi
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø Njia
ya haja kujaa damu
Ø Madoa
ya damu kwenye utumbo
Ø Madoa
madogo ya rangi nyeupe na nyekundu sehemu ya nje ya utumbo
Ø Madoa
ya rangi ya kijivu sehemu ya ndani ya utumbo
Ø Utumbo
mkubwa mpaka sehemu ya kutolea haja imevimba na kuwa ngumu
Ø Sehemu
ya chini ya utumbo mdogo imevimba na kuwa ngumu
Ø Utumbo
kujaa uchafu wa rangi ya kijivu na kahawia
Tiba
Ø
Amprolium
hydrochloride
Ø
Sulfa
Ø
Pata
ushauri wa daktari
Kuzuia na Kinga
Ø
Maranda na aina nyingine za malalo yawe makavu wakati wote.
Ø
Fuga kuku kwenye mabanda yenye sakafu isiyo na matundu
Ø
Vyombo vya chakula na maji visiwekwe chini, vining’inie juu ya
sakafu kuzuia kuchafuliwa na kinyesi
Ø
Banda lisiwe na msongamano mkubwa wa kuku
Ø
Weka utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi , wageni na ndege
hawaingii hovyo kwenye shamba/banda
Ø
Angamiza mizoga yote kwa njia stahiki kwa kuchoma moto au kufukia
kwenye shimo refu ardhini. Pia na maranda na vifaa vilivyochafuliwa vichomwe.
Ø
Kutumia dawa za tiba kwa ajili ya kinga.
Hii ifanyike kwa muda mfupi kuepuka kuleta usugu wa vimelea. Pata
ushauri wa daktari
HISTOMONASI
(HISTOMONIASIS)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na Protozoa ambao
hushambulia zaidi bata mzinga, kuku wanaweza kuwa na vimelea lakini hawaonyeshi
dalili, ijapokuwa pia wanaweza kuathirika. Bata na kuku wadogo ndio
wanaoathirika zaidi.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø
Maambukizi huenea kupitia kinyesi cha bata wagonjwa kuchafua maji
na chakula, udongo, na maranda
Ø
Njia kuu ya maambukizi ni kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa
na Protozoa
Ø
Maambukizi yanaweza pia kupitia kwenye yai na kifaranga kuanguliwa
kikiwa na ugonjwa.
Dalili
Ø
Kichwa kinageuka rangi na kuwa cheusi
Ø
Kinyesi cha njano
Ø
Kinyesi kugandamana kwenye njia ya haja
Ø
Mara nyingi vifo huwa vingi
Uchunguzi wa
Mzoga
Ø
Utumbo mkubwa kuvimba na kuwa na vidonda
Ø
Utumbo mkubwa wenye rangi ya kijivu na njano, na unaweza kuwa na
damu
Ø
Maini yana vidonda vya duara vyenye rangi ya njano na kijani
Ø
Uvimbe wa utandu unaozunguka utumbo iwapo vidonda vitatoboa utumbo
Tiba
Ø
Dawa
aina ya Salfa kuwekwa kwenye maji au chakula. Dawa hizi ni kwa ajili ya
tiba na kuzuia.
Kuzuia na Kinga
Ø
Bata mzinga na kuku watenganishwe wawe katika mabanda tofauti.
Ø
Weka utaratibu wa kuhakikisha wageni hawaingii ovyo kwenye
shamba/banda
Ø
Wageni wote wachovye viatu kwenye maji yenye dawa wakati wa
kuingia na kutoka shambani
Ø
Weka utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa
kwenye mabanda kabla ya kuingiza bata/kuku wapya
Ø
Hakikisha vyakula na maji hayachafuliwi na kinyesi
Ø Tumia
dawa za minyoo kudhibiti minyoo ya utumbo mkubwa ambayo ndiyo inayoeneza
ugonjwa. Pata ushauri wa daktari.
MINYOO
YA KUKU
Maelezo
Minyoo huishi katika njia ya chakula kwenye
kuku na wanyama. Minyoo inaweza kuwa na faida kwa mnyama au inaweza kuleta
madhara. Minyoo mingi ya kuku husababisha madhara. Minyoo muhimu katika kuku ni
aina ya Minyoo Bapa na Minyooya Duara.
MINYOO
BAPA (TAPE WORM INFESTATION)
Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na Minyoo Bapa
ambayo hushambulia kuku, kanga na njiwa. Minyoo huathiri kuku na ndege wadogo
na wakubwa ijapokuwa ndege wadogo wanaathirika zaidi.
Jinsi Ugonjwa
Unavyoenea
Ø
Maambukizi huenea kupitia kinyesi cha kuku, ndege na wadudu wa
kati (minyoo ya kwenye udongo,
kombamwiko, na
panzi).
Ø
Njia kuu ya maambukizi ni kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa
na wadudu wa kati wanaoneza
minyoo.
Dalili
Ø
Minyoo bapa (tegu) huishi tumboni na huweza kuziba utumbo na
kusababisha kifo
Ø
Kuku kukonda na kutokukua vizuri
Ø
Kuku wanaonyesha ukosefu wa damu – macho na ndimi na sehemu zisizo
na manyoya hupauka
Ø
Kuhara damu
Ø
Kwa kawaida vifo huwa vingi
Tiba
Ø
Dawa za Minyoo – huwekwa kwenye maji au chakula.
Ø
Pata
ushauri wa daktari.
Kuzuia na Kinga
Ø
Mabanda yajengwe na wavu kuzuia wadudu kuingia.
Ø
Pulizia dawa za kuua wadudu kwenye mabanda
Ø
Kinyesi cha kuku kikusanywe mara kwa mara na kusambazwa juani ili
kikauke na kuua lava.
Itaendelea.... Mawasiliano na mtaalam 0753226538 kwa msaada zaidi..
1 comment:
Everything is very open with a very clear explanation of the issues.
It was really informative. Your site is useful.
Many thanks for sharing!
My web page ... free music downloads (twitter.com)
Post a Comment