Translate this blog in your favourable language

Tuesday, November 23, 2010

USHAURI WA BURE KWA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA. Bongo flava…….

view of the day..


steve used to say.....
Kauli za wakongwe zilizo wahi kutolewa na wanamuziki wazamani zisipuuzwe kirahisi kama ambavyo watu wengi hasa wasanii wa bongo flava wanavyochukulia inawezekana ukasikia kauli halafu ukaipuuza lakini maneno yaliowahi kutolewa na akina nyoshi na mzee gurumo yasichukuliwe kama maneno ya watoto wadogo japo sasa kwa kiasi Fulani bongo flava inakua na ile dhana ya kua ni bazooka sasa inaelekea kupungua japokua  baddo tuna mziki wa kuiga kutoka magharibi ila haijarishi pia cha kuiga tukidumishe kiwe chute…
Mwanamuziki nguli katika   (prof.jay na ay ni waasisi wakubwa pia katika muziki wa bongo flavour natambua mchango wao wa mfano)            


miondoko ya dansi nchini Tanzania na anayeheshimiwa sana Maalim Ngurumo alikaririwa akisema wanamuziki wa kizazi kipya ni kama pipi aina ya"bazoka" na wengi wao wanakaribia kuisha utamu kwani wananoga mara moja tu halafu basi.Ngurumo hakuyasema maneno haya kwa mzaha kwani ni mtu anayeheshimika kimuziki na hata kiumri na kwa hivyo maneno yake lazima yachuliwe kwa uzito unaostahili na sio juu juu tu. Maneno haya mazito aliyoyanena Mzee Ngurumo kutokana na baadhi ya tabia za wanamuziki wenyewe yaliwachefua vilivyo  baadhi ya wanamuziki wakongwe katika muziki wa kizazi kipya,kati yao ni Prof Jay na AY ambao walipinga kauli hiyo kwa kusema sio ya kuwatakia mema lakini walishindwa kumpinga moja kwa moja Ngurumo kwani waliona ukweli ndani ya maneno yake na kuongezea kusema ni kweli baadhi ya wanamuziki wachache ni lazima wajiandae kwanza kabla ya kufikiria kuingia kwenye fani kwa kukurupuka na kutoa "Singo"
 Huu ni mwanzo wa makala bongo flava na hakika lazima tutazame tulipotoka tulipo na kasha tupange yanayokuja kwani hayo ndio ya msingi kuliko yote kwetu.. kama unabisha basi huwezi kufanikiwa ..
Makala ya steven mruma..

Post a Comment

Google+ Badge