Translate this blog in your favourable language

My pager view

Thursday, December 30, 2010

UZINDUZI WA ALBAMU YA TID WAFUNIKA ZOTE ZA 2010 KAMA ULIKOSA BASI USIKOSE ALBAMU HII YA MFANO.


hapa walioshirikishwa katika wimbo uliobeba jina la albamu wa sifai.
mwanaume wa shoka alieonja ladha ya jela
Kama ulikua bado hujui haya nikwambiayo basi chukua hiyo  huyu ni masanii pekee wa mziki wakizazi kipya namaanisha bongo flava ambae amepitia hatua ya kiume ya kuonja japo kidogo ladha ya jela kama kwa akina 50%, lili wayne, akon nk. namkubali mimi pamoja na watanzania na mamilioni duniani kote na kilichofanya mpaka naamua kuandika makala hii ni uzinduzi wa albamu yake mpya ambao uzinduzi huo naweza nikasema ulikua ni moja kati ya uzinduzi bora kuliko yote ndani ya 2010 nilishuhudia wasanii kibao wakimpa shavu wakiwemo akina ngair, Kelvin mshindi wa big braza 2009 na wasanii wengine kibao na staili alionyoa ilikua ni ya kiubunifu na kama ilikua ya kiduku style laniki alizidi ubunifu na kuwa kivutio kikubwa sana ndani ya billicanas hakika kwangu hakuna kama TID AMBAE NDIE NINAYE MZUNGUMZIA HAPA
HISTORIA NA KIMUZIKI HASA ALIPOTOKA…..
TID katika pozi
Jina lake halisi ni Khalid Mohamed a.k.a TID yaani Top In Dar na si yeye anayejiita hivyo bali wapenzi wake TID  alisoma shule ya msingi Bunge na elimu ya sekondari alienda kuipatia pale Shaban Robert iliyopo ndani ya City la Dsm.
Hapa tid anaelezea historia yake kidogo kimuziki hasa alipotokea  |”nanukuu;;; Unajua tangu niko mdogo nilikuwa napenda sana kusikiliza pamoja na kujaribu kuimba nyimbo
mbali mbali....lakini baada ya kuwa mkubwa na kuanza kujishughulisha na shughuli hizi za muziki ndipo wazazi wangu waliponikumbusha kuwa fanii hii nilikuwa nikiipenda sana toka nipo bwana mdogo ile mbaya hapo ndipo nilipojua kuwa kipaji changu kilianzia mbali sana.

.....Ila nilianza kuimba rasmi mwaka 1996 nilipokuwa nipo shule pale Shaaban Robert nikiwa na wenzangu kama David a.k.a Wabaki, Saitana na Dingo Jango ambapo tulianzisha kundi letu lililoitwa Black Gangster na mara nyingi tulikuwa tukiperfom kwenye concerts za kishule na 'Talent Night ' ambazo tulishinda mara kibao. Yap mwaka 1998 tulirekodi albam iliyojulikana kwa jina la Mission Impossible iliyokuwa na nyimbo 12 na ambazo ziliimbwa kwa 'Ngeli' kimombo mzee hahaha. mwaka uliofuata yaani mwaka 1999 nilishirikishwa kwenye nyimbo ya 'Anza wewe' na kundi la Joint Mobb nyimbo ambayo ilikuwepo kwenye albam yao ya 'Kitinda Mimba'. Vilevile nimeshashirikishwa pia kundi la CBM Crew katika Track yao 'My Girl Friend' na mwaka 
hapa makamuzi ya uzinduzi na AY

2000 nikaanza rasmi maandalizi ya Albam yangu.
Mwaka 2001 Crazy GK akanishirikisha kwenye Track yake 'Tutakukumbuka' na 'Malaika' ambazo zote zinapatikana kwenye albam yake inayokwenda kwa jina la 'Nitakupa Nini Mama' na mwaka huo huo nikafeat na kundi la Taqwa ndani ya nyimbo Maovu na Bongo Chelea Pina na Bongo
Chelea pina ambayo inapatikana katika Compilation ya BNa mwaka huo wa 2001 ndio nikaingia mkataba kama Solo Artist na Studio ya Poa Records iliyo chini ya Producer Amit a.k.a Mental ambapo sasa narekodi albam yangu itakayokuja kwa jina la Sauti ya Dhahabu na itakuwa na jumla ya nyimbo 9 kati ya hizo ni pamoja na Mrembo, Zeze, Hii Mic, Ukweli na nyingine ambazo sitazitaja sasa hivi.ongo Records ya mwaka huo  huyu ndie tid kwa kifupi akielezea wapi hasa alipotoka hapa alikua akikaririwa na media moja hapa Tanzania
logo yake muhimu ya kiburudani
NA KAMA UKIKOSA ALBAMU YAKE UTAKUA UMEKOSA MAMBO MENGI SANA NA UTAKUA BADO HUSTAHILI KUWA MDAU WA MZIKI POPOTE DUNIANI PATA KOPY HALISI UINUE MZIKI WA BONGO NA UMUINUE NA TID KATIKA GEMU… PAMOJA SANA
STEVENN MRUMA

Thursday, December 23, 2010

KRISMASI SIKUKUU AMBAYO INAHISTORIA NDEFU SANA NA INAYOPEWA NAFASI KUBWA NA WAUMINI WA KIKRISTO DUNIANI..

NA HII NI HISTORIA FUPI YA SIKUU YA KRISMASI WAPI HASA ILIPOANZIA NA ILITOKANA NA NINI...

Krismasi

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambako Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki  halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma na kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya Sikukuu ya Krismasi.
Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200. Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria (kitabu cha Stromateis I, xxi) alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.
Labda kadirio la tarehe ya Desemba 25 pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya kuzaliwa kwake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.
Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kuchukua nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus". Lakini pengine mambo yalikwenda kinyume, yaani kwamba Makaisari walianzisha sikukuu hiyo halafu wakaipanga tarehe ya Krismasi ili kushindana na Ukristo uliokuwa bado chini ya dhuluma.
Aliyeingiza sikukuu ya Kuzaliwa Jua (Mitra) huko Roma ni Eliogabalus (kaisari kuanzia 218 hadi 222). Baadaye Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273, hatimate ikahamishiwa tarehe 25 Desemba. Wakati wa Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba. (Taz. maandishi yaliyotajwa na Allan S. Hoey katika ukurasa 480 (rejeo 128) wa Official Policy towards Oriental Cults in the Roman Army, Transactions and Proceedings of the American Philological Association (70) 1939, pp 456-481).
Kutoka Roma, uliokuwa mji mkuu wa Dola la Roma, sherehe ya 25 Desemba ilienea kote katika Ukristo.

Wakristo wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki, Waprotestanti, sehemu ya Waorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda 

Habari za Krismasi katika Korani

Korani pia ina habari za kuzaliwa kwake Yesu (nabii Isa).
Sura ya tatu (Al Imran, 42-47) ina habari za tangazo la malaika kwa Bikira Mariamu zinazofanana na Luka 1.
Sura ya 19 (Mariamu, 16-34) inarudia tangazo la malaika kwa Mariamu na inasimulia kuzaliwa kwake Yesu chini ya mti wa mtende, halafu majadiliano kati ya Mariamu na ndugu zake. Mtoto mchanga Yesu akaanza kusema wakati wa kuzaliwa akimtetea mama yake dhidi ya ndugu zake. 
makala hii fupi kupitia vyanzo mbalimbali imehaririwa na steven mruma..

Wednesday, December 22, 2010

CHRISTMASS INAKUJA JE WAJUA HISTORIA YAKE? KAMA ULIKUA BADO KUA NAMI IKO NJIANI



kwa ufupi sana hii ni sherehe ambayo huadhimishwa kila desemba 25 na inamana kua yesu kristo kwa wakristo amezaliwa...
Christmas
Christmas
Christmas decorations on display.
Also called Christ's Mass
Nativity
Noel
Feast of the Nativity
Observed by Christians
Many non-Christians[1]
Type Christian, cultural
Significance Traditional birthday of Jesus
Date December 25
January 6 (in Armenia)
January 7[2] (in a minority of Eastern Orthodox churches)
Observances Gift giving, church services, family and other social gatherings, symbolic decorating
Related to Annunciation, Advent, Epiphany, Baptism of the Lord
sasa subiria habari kamili
na steven..

MFAHAMU KWA UFUPI RAPA WA WEST COST ANAETIKISA HADI LEO SNOOP DOGGY


Cordozar Calvin Broadus, Jr
HAPA NI HISTORIA YAKE KWA UFUPI HASA ALIPOTOKEA

Snoop Doggy

Cordozar Calvin Broadus, Jr (amezaliwa, 20 Oktoba 1971) ni Rapa wa kimarekani na pia muigazaji wa filamu. Alipata umaarufu kama Snoop Dogg, mwanzoni walikuwa wakimuita Snoop Dogg Doggy.
SNOOP DOGGY

Akiwa anawakilisha kikosi cha West Coast Hip Hop, pamoja na mshirika wake wa karibu bwana Dr. Dre ambaye ndiye aliyesababisha Snoop kuwa hapo alipofikia. Snoop kuna misemo yake ambayo imezoleka sana midomoni mwa watu vile akisema 'fo' Shizzle, manizzle, akimanisha, kweli ndugu yangu, useme huo ulibuniwa na mwanamuziki mmoja wa huko huko nchini marekani maarufu kama Frank Smith & the Band, mnamo miaka ya 80 hivi

  Maisha ya Mwanzo

Snoop alizaliwa mjini Long Beach, California tar. 20 Oktoba 1971. Akiwa bwana mdogo alipata jina la Snoop ambalo alipewa na mama yake mzazi kama jina la utani kwakuwa alikuwa anapenda kutazama kipindi cha televisheni kilichokuwa kinaitwa "Peanuts", kipindi ambacho kiliegemea kwenye masuala ya "Ucheshi", likiwemo na jina fulani la Snoop Dogg.
Snoop ajiunga na shule ya Long Beach Polytechnic High School, na baadae akapelekwa jela kwa kujishughulisha na maswala ya uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya. Snoop pia alikuwa mmoja wa wanachama wa kikundi kidogo cha kihuni kilichokuwa kinaongozwa na "Bow Keene Mundine" ndani ya Long Beach.
Jina la Kiraia
Mwanamuziki Snoop akiwa Mjini HawaiiCordozar Calvin Broadus, Jr
Jina la kisanii
Snoop Doggy Dogg
The D O Double G Bigg Snoop Dogg Tha Bigg Boss Dogg
Nchi
Alizaliwa
Aina ya muziki
Rap na Hip Hop
Kazi yake
Mwanamuziki, Muigizaji, Mtayarishaji
Miaka ya kazi
mn. 1992 -
Ameshirikiana na
Ala
Sauti, Gita,Kinanda,Kinakilishi
Kampuni
Death Row, Interscope, Universal, No Limit, Priority, TVT, EMI, Star Trak, Geffen, Doggystyle

Monday, December 20, 2010

kupatwa kwa mwezi na jua [solar and lunar eclipse] matukio ya kawaida sasa duniani

leo itatokea kupatwa kwa mwezi usiku na hili ni kutoka kwa watbiri wa hali ya hewa 

 katika habari za kitabiri leo jumatatu kutatokea kupatwa kwa mwezi na hii imenifanya nikumbushie matukio haya ambyo yalitabiriwa kama ndio dalili za mwisho wa dunia na hali hii ya kupatwa kwamwezi ni yakawaida kabisa hapa duniani...

Kupatwa kwa jua kunatokea wakati mwezi unafunika jua. Tokeo lake ni kupungua kwa jua hadi kutoonekana tena na kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu.  Misingi ya kupatwa kwa jua
Kupatwa kwa jua kunatokea kama dunia, mwezi na jua zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua. Katika hali hiyo kuna kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia. Kivuli hiki hakifuniki dunia yote. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua             
Aina za kupatwa kwa jua
Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa jua.
  • kupatwa kabisa: jua lapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.
  • kupatwa kipete: mwezi huonekana mdogo kuloko jua. Kwa hiyo duara ya kung'aa ya jua ni kubwa kuliko duara ya mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete.
  • kupatwa kwa jua kisehemu: Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu hona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. Wakitazama jua kwa filta kwa mfano kioo kilichopakwa dohani katika moshi ya mshumaa huwa wanaona sehemu ya duara ya jua imefunikwa. 
KUPATWA KWA MWEZI
H hutyokea pale dunia inapokua katikati ya jua na mwezi na kufanya mwezi ushindwe kuakisi mwanga kutoka kwenye jua ikumbukwe kua mwezi hupata ama huakisis mwanga wake kutoka kwenye jua sasa dunia inapokua katikati mwanga wa jua haufiki katika mwezi na kusababisha mwezi kua na giza na hii haichukui muda mrefu kisha hali huwa kama kawaida na matukio haya hutokea mara kwa mara sasa duniani na limekua kama jambo la kawaida kabisa