Utangulizi
Ufugaji wa kuku ni njia rahisi ya kujipatia kipato na lishe bora kwa kaya nyingi za vijijini.Hii ni kutokana na ukweli kwamba:
• Ufugaji hauhitaji mtaji mkubwa kuuanzisha.
• Ni rahisi kuusimamia.
• Faida inapatikana mapema.
• Mali ghafi nyingi zinazohitajika zinapatikana kwa urahisi katika mazingira ya vijijini.
• Kwa kipindi cha hivi karibuni, uzoefu unaonyesha kuwa soko la kuku wa kienyeji
linakua na linaelekea kwenye kutokutosheleza wateja.