Translate this blog in your favourable language

My pager view

Sunday, December 25, 2016

The Contents of Cattle Diseases and Conditions of Campylobacter infection (Vibriosis)



Campylobacter infection (Vibriosis)

  The NADIS data show that abortion and infertility remain significant problems on farm. One of the most important causes of infertility and abortion in UK cattle is infection by Campylobacter fetus. This organism can cause sporadic abortion, abortion storms, metritis, delayed return to heat, and very low pregnancy rates.

How do cows get infected?

Monday, June 27, 2016

NGUGI WA THIONG`O: WASOMI NA VIONGOZI WA SERIKALI WA AFRIKA WATEKWA NA FIKRA ZA KIGENI.


 


 Credit, Habari  kwanza.

Mwanazuoni mkongwe na mwanafasihi wa lugha za Kiafrika aliyebobea duniani, Profesa Ngugi wa Thiong’o amesema si viongozi wa serikali za Afrika pekee waliotekwa na fikra za kigeni, bali hata wasomi wa karne ya sasa ni majemedari wanaopigana vita katika kambi ya adui.
Amesema majemedari hao tena wakiwa na majina ya kizungu na kuweka kando ya asili, wanaona fahari kutumia lugha za kigeni kama silaha ya maendeleo, bila kujua kuwa wanaangamizwa wao na vizazi vyao na kuendelea kujenga matabaka makubwa, huku akisisitiza kuwa mtu anayedharau lugha ya mama yake, hata angejua lugha zote duniani, ni mtumwa.
Profesa Ngugi alisema hayo jana, alipokuwa akitoa mhadhara wa kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, kwenye ukumbi wa Nkrumah, siku moja kabla ya chuo hicho leo kumtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari katika Fasihi.
Ikiwa ni mara yake ya kwanza kutoa mhadhara duniani kwa lugha ya Kiswahili, Profesa Ngugi alisema: “Lugha imekuwa uwanja wa vita baina ya mtumwa na mtawala, ni silaha ya kutamalaki na kupinga kutamalakiwa kama silaha ya upanga, lakini Waafrika wengi tunaziweka lugha zetu za asili kwenye uduni na kutukuza za kigeni, tumesahahu hata majina yetu ya asili na kutukuza ya kigeni.
Profesa Ngugi ambaye jina lake la ubatizo ni James, ambalo aliliacha na kutumia Ngugi wa Thiong’o akitambulisha uafrika wake, alisema Bara la Afrika ni kubwa duniani, lakini limeendelea kutawaliwa kifikra, nje watu wanajiona Waafrika lakini katika akili kwenye bongo zao ni Wazungu kiutawala, kiutendaji na kisiasa, hali inayojenga matabaka makubwa.
“Majemedari wa Afrika wanaotazamiwa kulikomboa Bara hili wametekwa katika kambi ya adui waliodunisha lugha zetu ili kujinufaisha, katika hili hakuna wa kujigamba, kwani si viongozi wa Serikali za kiafrika wala wasomi, wote wametekwa, sasa wewe umetekwa unamwongozaje mtu, utampeleka wapi?,” alihoji Profesa Ngugi na kushangiliwa na hadhara kubwa iliyofurika katika ukumbi wa Nkrumah kumsikiliza jana.
Akifafanua kitaaluma, Profesa Ngugi alisema wasomi na viongozi wa Serikali wanalazimika kuiangalia Afrika kama watalii au wageni huku akidai wasomi wanaficha vito vya thamani walivyopata kwa kujua lugha za Kiingereza na Kifaransa wanazopaswa kuziwasilisha kwa lugha zao za kiafrika wakidhani wanamkomoa mtu kumbe wanajikomoa wenyewe
“Kuna tunu nyingi lakini tunazificha katika lugha za kigeni, ni mzaha kitaaluma kama si upumbavu kuona lugha yako mama ni duni, unalifanya Bara lako lionekane duni mbele ya mabara mengine, tulitendewa hivi na visiwa wa Ulaya, sasa tunajitendea wenyewe, hali hii lazima ibadilike,” alisisitiza Profesa Ngugi anayekumbukwa kwa utunzi wa vitabu vingi vya Fasihi duniani kikiwamo cha The River Between.
Profesa huyo aliyepata kutunukiwa shahada za heshima za udaktari zaidi ya saba katika vyuo mbalimbali duniani hadi sasa - ya leo ikiwa ya nane- alisema lazima asasi za kitaaluma, taasisi za kitaaluma na wasomi kwa kushirikiana na Serikali kujenga nguvu ya pamoja kuwezesha lugha za kiafrika kama Kiswahili kuwa silaha ya mapambano dhidi ya ukoloni mamboleo.
Alisema kwa sasa Afrika inahitaji serikali zenye sera ya kukuza lugha za Afrika kama za aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambao Profesa Ngugi aliwanukuu kama wanazuoni waliokombolewa kifikra tofauti na wa sasa ambao wote ni mateka.
“Hatuhitaji viongozi mateka kwa sasa, Kiswahili kinapaswa kuwa mstari wa mbele katika vita hii, kinapaswa kuwa lugha ya dunia kwa sasa, hakuna aliyekufa kwa kuongea Kiswahili na kupata haki ya kuishi kwa kuwa anaongea Kiingereza ama Kifaransa,” alisema Ngugi anayeishi uhamishoni Marekani na kuongeza:
“Kufaulu kwa Kiswahili leo ni matokeo ya wasomi wa kwanza waliohitimu kwa lugha za kigeni na kurejesha thamani ya kutekeleza walichokipata kwa lugha zao za asili, Nyerere alipohitimu Chuo Kikuu cha Makerere enzi hizo kikiwa cha London, aliweka sera kukipa hadhi Kiswahili, hii inathibitisha kwamba lugha za Afrika zinaweza kukuza fikra kama lugha nyingine duniani.”
Profesa Ngugi alisisitiza, kuwa hakuna haja kwa wasomi kukwepa wajibu na mapambano haya kwa kuwa wao ndio wanaotarajiwa kufungua njia na kuongeza kuwa wasomi wa zama za sasa wanakimbia mapambano na kusahau kwamba “wageni wametupa lafudhi zao na kujiona bora tunapozungumza kwa mtiririko wao, wakachukua rasilimali zetu na kutuwekea kinyaa kuzungumza lugha zetu”. 
Alisema si vibaya kujua lugha nyingi kadri iwezekanavyo, lakini ni kosa lugha ngeni zikachukua nafasi na utukufu wa lugha za asili.
Alishangaa baadhi ya utumwa wa sasa ulivyokomaa katika kutukuza Kiingereza na kueleza namna ambavyo baadhi ya shule watoto huchapwa wakizungumza lugha za asili na kutukuzwa wanapozungumza Kiingereza.
“Huu ni wakati wa Afrika kuchagua kujiweza ama kuwezwa, kuna watu wanafikiri kwamba Mungu anaongea Kiingereza pekee ama Kifaransa, lugha nyingine hasikii, hapana, lugha zote zitatupeleka mbinguni, naomba niwaache na neno hili; ukijua lugha zote duniani na hujui lugha ya mama, wewe ni mtumwa na umewezwa, ukijua zote na ya mama pia, wewe u huru na umejiweza,” alisema Profesa Ngugi.
Awali, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, akimkaribisha Profesa Ngugi kuzungumza, alimwelezea kama mwanazuoni, mwanafasihi na mwanamapinduzi aliyepigania uhuru kifikra na uhalisia, kupitia kalamu yake na uwezo wake na ni urithi mkubwa kwa Bara la Afrika.