Translate this blog in your favourable language

Sunday, December 5, 2010

CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO NA WAPI TUNAPOJIKWAA NA SABABU AMBAZO HUHARIBU MAHUSIANO KWA HARAKA SANA..

Kati ya shughuli nzito ambazo huwakumba watu walio katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa ni kuhakikisha kuwa mahusiano yao yanakuwa imara. Ni shughuli yenye changamoto nyingi kwani huhitaji uwiano, maana mwanamume na mwanamke wameumbwa tofauti na kila mmoja ana matakwa na matarajio yake.
Sababu za kuvunjika kwa uhusiano zinaweza kuwapo nyingi na kutofautiana kutoka uhusiano huu na ule, lakini zipo kumi ambazo zinaweza kuchukuliwa kuwa kuu. Ukizifahamu utajua jinsi ya kuboresha uhusiano wako wa sasa au baadaye, au kukuweka sawa kisaikolojia kwa ajili ya uhusiano mpya.

SABABU HIZI ZINASABABISHA MAPENZI KUVUNJIKA MAPEMA


1.WIVU ULIOKITHIRI
Wivu ni mojawapo ya sababu kuu za kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi au hata ndoa. Wivu wa kupindukia unaweza kusababisha ugomvi ambao nao ni sababu kubwa ya kuachana kwa wapenzi.

Wivu husababishwa zaidi na kutokujiamini kwa mtu. Kwa hiyo, ili kuepuka wivu na
kuunusuru uhusiano wa kimapenzi, lazima mtu kwanza ajithamini na kujiamini kuwa
anastahili kupendwa na mpenzi wake kama alivy0

2.MAWASILIANO HAFIFU

Mawasiliano ni kitu muhimu sana katika mapenzi. Iwapo wapenzi watashindwa kuelezana hisia zao, mawazo yao, mitazamo yao, imani zao, matatizo yao au hata furaha zao, uhusiano utakuwa unaelekea pabaya.

Inapotokea hiyo ikawa sababu ya kuachana kwa wapenzi, basi mtu anapojifunza tena
kupenda atapaswa kujifunza pia jinsi ya kuwasiliana vema na mwenzake, kwani kwa
hakika mawasiliano mabaya ni sababu kubwa ya kuachana kwa wapenzi..


3.KUMNYANYASA MPENZI WAKO BILA SABABU.
Hii ndiyo sababu ambayo pengine iko wazi zaidi. Kuna aina mbalimbali za unyanyasaji
ambao hujitokeza baina ya wapenzi na si lazima kwamba mwanamume ndiye anayemnyanyasa mwanamke kama ilivyozoeleka. Hata wanawake huwanyanyasa wanaume.

Unaweza kudhani ukinyanyaswa tu na mpenzi au mwenza utamwacha, lakini ukweli ni kwamba wengi huvumilia, pengine kutokana na kuiogopa jamii inayowazunguka. Lakini ukweli ni kwamba unyanyasaji huondoa kabisa maana ya mapenzi na kusababisha wapenzi
wengi kukosa sababu ya kuendelea kuwa pamoja.
KUKOSA UAMINIFU HASA UNAOTOKANA NA TAMAA ZA KIJINGA
Kushindwa kutimiza ahadi, kusema uwongo au kufanya usaliti wa kimapenzi ni mambo
ambayo humwondolea mtu uaminifu kwa mwenzake. Kwa hakika, kukosekana kwa uaminifu ni sababu kuu ya kuyumba na hata kuvunjika kwa mahusiano yaliyo mengi.

Iwapo kuaminiana kwa msingi kabisa katika uhusiano kutavunjwa mara kwa mara, hasira za mpenzi kwa mwenzake zitalimbikizwa na hamu ya wapenzi/wenza kuendelea kuishi pamoja itapungua. Wapenzi walio katika uhusiano wenye mizizi na afya njema wanaweza kukubaliana kumaliza tofauti zao na kusonga mbele. Kama wataheshimu ahadi na viapo vyao vipya mambo yataendelea.

Kumdanganya mpenzi mara kwa mara, kumsaliti mara kwa mara na kuvunja ahadi zako mara kwa mara huufanya uhusiano kudhoofika na hatimaye nguzo yake muhimu – yaani kuaminiana – kuanguka. Hapo ndipo uhusiano hufika kikomo.
  Iwapo itatokea kuwa mmoja wa wapenzi/marafiki au wote wawili akawa hajitambui na kufuata matakwa yake, mahitaji yake, matamanio yake, mipango yake ya baadaye, malengo yake, msimamo wake, hulka yake na vipaumbele vyake, haitakuwa rahisi kwa watu hawa wawili kuwa na uhusiano wenye afya.5.. KUJITAMBUA NA KUTAMBUA MAJUKUMU YAKO.
Kujitambua huwasaidia wapenzi kuwa huru kila mmoja kwa mwenzake, akimweleza anataka nini, jambo ambalo husaidia kuimarisha uhusiano. Lakini inapotokea kuwa mmoja wa wapenzi hajitambui, au wote wawili hawajitambui, ni rahisi sana uhusiano kuvunjika, hasa kama wahusika waliingia katika uhusiano huo wakiwa na umri mdogo.lazima utambue kuwa unahaki gani na wajibu gani kwa mpenzi wako nae akitambua haki na wajibu wake katika mahusiano lazima yatadumu ila ikiwa nin kinyume na hapo hakuna penzi litakalo dumu daima..
                                   USHAURI WANGU KWAKO
NIVYEMA SANA UKAJARIBU KUSOMA NA KUANGALIA WATU WANAISHIJE KATIKA MAHUSIANO WA WAPI WANAANGUKA NA WAPI WAFANIKISHA HALAFU TAMBUA WAJIBU WAKO KWA MWENZI WAKO KABLA YA KUMKABIDHI MOYO NA BILA SHAKA LAZIMA UJUE KUZISOMA NYAKATI NA PIA KUBALI KWENDA NA MABADILIKO.. TAMBUA YAKUA MAPENZI SIO JAMBO LAKITOTO  NI KITU AMBACHO KIPO DEEP SANA NA KINAHITAJI UMAKINI PIA UMAHILRI SANA KUWEZA KUONGOZA VINGINEVYO KILA SIKU UTALIA NA UTAJUTIA NA LADHA YA MAPENZI ITAKUA CHUNGU KWAKO DAIMA...
 STEVEN M..
 MWISHO
Post a Comment

Google+ Badge