Translate this blog in your favourable language

Friday, January 4, 2013

Rais Kikwete aongoza mamia kumzika Sajuki

RAIS Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya Watanzania katika mazishi ya aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Juma Kilowoko maarufu kama (Sajuki), katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete alifika katika makaburi hayo mapema kabla ya mwili wa marehemu kuwasili na kukaa katika viti vilivyokuwa vimeandaliwa maalum kwa ajili yake.
Rais Kikwete alimfariji Baba mzazi wa marehemu mzee Kilowoko pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifwamba.
Mbali na Rais Kikwete kushiriki katika maziko hayo pia alikuwepo Meya wa Jiji la Ilala Jerry Silaa pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Msanii huyo wa Filamu  nchini alifariki Dunia juzi alfajiri kwenye Hospitali ya Taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.Sajuki ameacha mjane na mtoto mmoja, wa miezi tisa
Baba mzazi wa marehemu Sajuki,mzee Kilowoko akiweka udongo kwenye kaburi la mwanaye.Picha zote na Jackson Odoyo
Rais Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la SajukiMwili wa marehemu Sajuki ukifunikwa ndani ya kaburi
Post a Comment

Google+ Badge