Translate this blog in your favourable language

My pager view

Thursday, February 9, 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011 CHANZO CHA SHULE ZA KATA KUFELISHA ...


baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mihani ya taifa
Katika hali ambayo itazoeleka kwa sasa ni hali ya kufeli kwa wanfunzi wengi sana hasa wanaosoma shule za sekondari za kata. na katika hangaika yangu huku na huku najua kabisa wizara inatambua sana tatizo hili lakini sijaskia ikitamka lolote katika kufeli huku kwa wanafunzi wa kidato cha nne hasa wanaosoma shule za kata ambazo nina uhakika ufaulu wa daraja la kwanza haufiki asilimia moja kwani katika shule zilizofanya vizuri kzribu zote ni shule za private na chache sana hasa za bweni na vipaji maalum kama ilboru, Galanos, Tabora boys, Lymungo kwa mbali nk. leo  jana na leo nimejaribu kuangali a  karibu shule mia tano kama sio mia sita zote za kata nimekutana na division one 5 tu na division two zipo 27 tu na divisoion three 48 tu huku division four zikiwa na nyingi sana lakini cha ajabu na ca kushangaza waliopata zero yaani 0 ni wengi kuliko waliopata nangalau division four ... vituko vilitawa ambapo wanafunzi wengi wlifutiwa matokeo yao na ni wengi sana na wote kwa kufanya udanganyifu mfano kuna mwehu mmoja kaandika mashairi ya mapenzi katika mtihani huu ni ni iujinga mabo niatauzungumzia katika muendelezo wa makala hii...
ufaulu ulikuwa ni kama ifuatavyo.
watahiniwa laki mbili na elfu 25 sa.wa na asilimia 53.37 wamefaulu huku kati yao wasichana ni elfu 90 na 885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni laki moja na elfu 34 sawa na asilimia 57.51.Shule ya sekondari ya wasichana ya St. Francis Mbeya imeongoza kwa shule kumi zilizofanya vizuri, ambapo katika wanafunzi waliofaulu vizuri sana wameongozwa na Moses Andrew Swai kutoka shule ya sekondari ya Feza iliyopo jijini Dar es salaam.

 lakini ukiangalia shule mia bora hakika huwezi kukuta shule ya sekondari ya kata wala ukiangalia zilizo felisha sana huwezi kukuta shule binafsi hii ni kwasababu ya mazingira ya elimu bora inayotolewa na shule hizo na kama serikali ingeboresha shule angalau kwa asilimia 50 labda tungefika mbalia sana. lakini hali ni tete sana kuko vijijini....

nini chanzo cha wanafunzi wote hao ambao hawana tena muustakabali wa maisha yao ya shule?
shule za kata ni...
Bila shaka swali hili halina majibu ya moja kwa moja kwasababu kuna changamoto kubwa sana ambazo kamwe bila mikakati mizuri tutajikuta wa vijijini watakuwa wanafeli palepale hasa washule za kata ambazo zipo mijini pia ila kwa changamoto tofauti kidogo... sababu za kufeli kwao nyingi nazijua nazo ni kama ifuuatavyo.....
    1. Sera mbovu kabisa za elimu hasa ya kujenga sekondari nyingi bila kuwa na uwezo wa kuzihudunmia.....
hili ni tatizo kubwa sana ambalo nimeliona niliwahi kuwa mwalimu wa shule moja ya kata kama mwalimu wa muda ikafika kipindi walimu wako semina inabidi watafutwe wanafunzi waliomaliza kidato cha nne wakafundishe katika ile shule. shule zipo nyingi walimu wachache vitendea kazi hakuna kama vitabu pamoja na maabara kwaajili ya masomo ya sayansi. hatawezi kupata mafanikio ya elimu kwa kuweka majengo mengi na kisha wanasiasa wanajisifu kuwa wanafunzi wengi wameingia sekondari kisha hawajui kama wanasoma au la huu ni ujinga wa makusudi sio kwamba hawajui....
ni wangapi wanapata fursa hii ya kusoma na kufaulu?
    2. mazingira magumu ya walimu pamoja na wanafunzi....
 nimekutana na changamoto nyingi sana katika maeneo ya vijijini ambayo nina uzoefu nayo sana  unakuta shule ya sekondari wanafunzi wanenda shule mda wanaoutaka kwasababu walimu hawafiki kazini kwa wakati na wanaweza kuondoka kituo cha kazi mda atakaojisikia na hili linasababishwa sana na wazazi na wanafunzi bila kusahau wanasiasa hasa madiwani
   3. Utovu wa nidhamu shuleni hasa suala la mapenzi.. 
katika mabo ya ajabu kabisa suala la mapenzi shuleni limekuwa jambo la kawaida sana na wala hata ikatokea walimu wakawa wanafahamu kuwa kuna  miongoni mwa wanafunzi wanajihusisha na suala la mapenzi hakuna hatua yoyote inayochukuliw a kuondoa hali hiyo ama kuwapa adhabu kulingana na sheria za shule... lakini baya zaidi walimu wengi kuwa na mahusiano na wanafunzi pamoja na wafanyabiashara wakubwa mabo pia wanachangia sana mimba shuleni.
hakuna jipya san ufaulu umeongezeka shule binafsi.
   4. Wanafunzi kuzoea mazingira ya eneo moja tu.
wanafunzi wamesoma kata na kijiji kimoja kisha anaenda sekondarui palepale hewezi kupata changamoto za kimaisha na kubadili mawazo kwa kuwa na kabila ama watu wa aina tofautoi na uliozoea kwani ujinga aliotoka nao shule ya msingi anaingia nao sekondari na wajinga wenzie walewale wa mtaani anakutana nao na hakika kusoma hapa inakuwa ishu ni bora kungekua na karatasi au fomu maalu amabyoi mzazi atajaza kama atakuwa na uwezo wa mtoto wake akipelekwa wilaya nyingine au mkoa mwingine atamudu gharama ili watoto hawa wapelekwe maenieo tifauti kubadili mawazo na kubadili mfumo wa maisha yao..

ukimaliza four kula zako bata basi
Kuna haja sasa serikali kupitia wizara ya elimu kubadili mfumo wa sekondari za kata kwa kijaribu kuwashift au kuwabadili maeneo ya kusoma wanafunzi wanaotoka shule za msingi hapo hapo kijijini na kuingia sekondari hapohapo kijijini ili kuabadili mfumo wa mazingira na hili lifanye kwa ushirikiano na wazazi pmoaja na walimu. pia iborteshe mazingira na vitendea kazi vya walimu  ikiwa ni pamoja na kufikiria upya kuwaongezea walimu mishahara hasa wale walio katika mazingira magumu ikiwamo kuwakopesha usafi kama pikipiki ili kumudu maisha yao ya kazi kwa ujumla.. mimi naona IPO HAJA YA WALIMU WOTE KUGOMA ILI KUONGEZEWA MSHAHARA MAANA NAO NI MOJA KATI YA KUNDI LINALO ISHI MAISHA DUNI SANA NADHA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU WAISHAWISHI SERIKALI IONGEZE MISHAHARA HATA KWA ASILIMIA 50. ILI KUWEZA KUKABILIANA NA MAISHA MAGUMU YA UFUNDISHAJI NA YA KIMAISHA KWA UJUMLA KAMA MADAKTARI WAMEGOMA NA WAMEONYESHA MSIMAMO KWANINI ISIWE KWA WALIMU PIA NA MADAKTARI MSIOGOMA MMEWASALITI MADAKTARI WENZENI KUMBUKENI MSHARA UKIPANDA UTAPANDA NA NYIE KUWENI NA MSIMAMO....
           Makala hii kama kawaida imeandikwa na Steven Mruma  bila ushawishi wa mtu yeyote na naupongeza mgomo wa madaktari unaoendelea maeneo mbalimbali hapa Tanzania.  Malizeni madokta walimu najua mnajiandaa bia kusahau idara mbalimbali kama za sheria watendaji nk....

                                                             MWISHO