Translate this blog in your favourable language

Monday, May 21, 2012

HABARI ZA MICHEZO ZA WIKI: AFRIKA MAJONZI, ULAYA CHEREKO. R.I.P. Mafisango Halaaa Chelsea.


                  
wakati hali ya tanzania ikiwa ni majonzi huko ulaya hali ya furaha imewatala mashabiki pamoja na timu nzima ya chelsea baada ya kufanikiwa kwa mara ya kwanza kutwaa taji la Uefa C. league baada ya kuizamisha Bayern Munich kwa Penalt 4 KWA 3 baada ya dakika 120 kumalizikwa kwa sare ya 1 kwa 1 baada ya Didier Drogba kusawazisha bao dakika ya 88. chelsea ni mara yake ya kwanza kutwaa taji hili huku kikosi hicho kikikikabiliwa na matatizo mengi sana ikiwamo ya kumtimua aliekuwa kocha wa timu hiyo Vilas Boas na kushilkiliwa na kocha msaidizi Di mateo na bado ikionekana kama si kitu lakini imedhihirishia ulimwengu kuwa ni moto wa kuotea mbali.


Mnamo tarehe 17 mwezi huu mchezo wa soka ulikumbwa na giza nene na simanzi kubwa baada ya kutokea kifo cha ghafra cha aliyekuwa mchezaji wa simba kiungo mahiri Patrick Muttesa Mafisango kilichotokea kwa ajali ya Gari maeneo ya chang'mbe jijini dar-es- salam mafisango ambeye amezikwa jana huko kwao kongo kinshasa amekumbwa na umauti siku chache kabla ya kuondoka yeye na Niyonzima Kuelekea kwa Rwanda katika timu ya Taifa aliyokuwa akiichezea kama timu yake ya taifa japo kuwa ni mzaliwa wa kongo. nikiwa katika pilikapilika za kazi na mambo mengine nilishtushwa sana na taarifa za msiba huo nilikuwa mbali na kwakweli ilipunguza hata ufanisi wa nlichokuwa nakifanya... alale pema peponi Petii mkambo Mutesa Mafisango..
Post a Comment

Google+ Badge