Translate this blog in your favourable language

Monday, April 2, 2012

USHINDI WA KISHINDO WA CHADEMA ARUMERU MASHARIKI HARAKATI ZA KUCHUKUA NCHI YETU KUTOKA KWA MAFISADI.

HONGERA NASARI
Katika mambo mambo ambayo yamenipa raha sana ni ushindi wa CHADEMA wilayani Arumeru kwa saasa mimi ni moja kati ya wakazi wa hapa arumeru maeneo ya Tengeru na nafurahia sana kuona harakati za wanaharakati wa kupinga ufisadi zinafanikiwa na hii ni njia ya kuchukua nchi yetu kutoka kwa mafisadi ambao wanaona raha kula jasho la mtanzania hasa mtanzania maskini. Ninaamini kabisa Tanzania Bila mafisadi inawezekana na inabidi tufanye kama ambavyo wana Arumeru wamefanya kwa kuiondoa nguzo nyingine ya kifisadi kama matokeu hayo yalivyotangazwa leo asubui
Hakuna ubishi 2015 ni CHADEMA.
Kwa Mujibu wa Matokeo ya liyotangazwa asubuhi hii yanaonesha kuwa Mgombea Ubunge wa Joshua Nassari CHADEMA amepata kura  32,972, na kumshinda Mgombea mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo, Sioi Sumari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 26,757.
Kwamatokeo hayo inafanya kuwa idadi ya Kura zilizompa ushindi  Nassari wa Chadema kuwa kura 6,215 dhidi ya Sioi Sumari CCM.
Msimamizi wa huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi.
Gagenzi pia ametangaza matokeo ya wagombea wengine ambao walitoka vyama vya Siasa nchini kuwa kama yafuatavyo:-
AFP – 139, DP -77, NRA – 35, SAU – 22, UPDB – 18 na TLP – 18.
Chukua baraka za kuwaua mafisadi
Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.
sasa mpaka kieleweke mwaka 2015 na natabiri kuwa nchi itarudi mikononi mwa watanzania wengi aambao wengi wao ni watu wa chini na wanamaisha duni sana. Joshua Nasari bado ni kijana na anauweza kuwepo katika uongozi kwa mda mrefu zaidi na hili linaweza kuleta manufaa katika nchi yetu kama atatumikia wananchi kama alivyo ahidi katika kampeni zake.  napendezwa pia na kauli walizotoa baadhi ya viongozi na watu maarufu na wadau wengi hasa katika facebook na twitter na wengi walisema yafuatayo....
Tunawashukuru wana Arumeru Mashariki kwa imani yao kwetu hasa kwa kijana Joshua Nassari. Ushindi wao ni ushindi wetu sote. HONGERA SANA JOSHUA. Mungu mbariki JOSHUA, Mungu ibariki Tanzania. haya yalikuwa ni maneno ya Dr. Slaa.
 
http://millardayo.com/wp-content/uploads/2012/04/Nape-Nnauye-April-2-2012.png 

Haya yalikuwa ya nape nuye na Zito kabwe kupitia face book. 
 HONGERA CHADEMA NA SASARI KWA KUKARIBIA KUICHUKUA NCHI YETU KATIKA MIKONO SALAMA  
MUNGU IBARIKI CHADEMA MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WAHUKUMU MAFISADI KWA FEDHEHA NA KWA KUSHINDWA KATIKA CHAGUZI ZOAO KAMA ILIVYOKUWA ARUMERU.
Post a Comment

Google+ Badge