Translate this blog in your favourable language

Saturday, April 7, 2012

REST IN PEACE WAJINA STEVEN KANUMBA [Matukio ya msiba katika Picha] WE ARE BACK YOUR

Mama wa Kanumba Flora Mwitegoa
Mama wa kanumba  awasili jijini dar es salam na pia adhibitisha kuwa mwanae atazikwa dar na atazikwa
 katika makaburi ya kinondoni siku ya jumanne.
                                 Steven kanumba na mama yake kushoto na Dotnata kulia

mama wa kanumba ( Flora Mutegoa) akiwa na huzuni kubwa baada ya kumpoteza mwanaye kipenzi Steven kanumba
Katika mahojiano yaliyofanyika Mama mzazi wa Steven Kanumba amesema angependekeza mwanaye azikwe jijini Dar es salam na aliskanusha taarifa kuwa mwanaye hana ndugu kwani yeye ndiye mama yake na kuna dada yake pia wapo ndugu wengi sehemu mbalimbali hapa Nchini.  na Taarifa zingine zinasema kuwa Lulu amekataa kutoa ushirikiano kwa Polisi Mpaka pale Mwanasheria wake atakapofika bado taarifa ya madaktari inasubiriwa na pia taarifa ya kipolisi kuhusiana na kifo cha Steven Kanumba Pichani hapo chini.

Tabasamu hili natumai utaingia nalo huko uliko kwasasa but duniani umetuachia simanzi kubwa sana kama kuna uwezekano wa kuwaona wasalimie Mzee kipara, mr Ebbo, complex na Vivian, john mjema, steve 2k, faza nelly nk.

baadhi ya watu maarufu na wanchi ndugu jamaa na marafiki walifika sinza kuwafariji waliofikwa na msiba huu mzito

Kila mmoja alikuwa anawaza lake na alikuwa na huzuni  kwa namna yake ni wazi msiba huu umemgusa kila mtu hasa kutokana na ughafra wake.

wasanii wengi walikuwepo Natasha ambaye walikuwa wote kaole na katika filamu nyingi walikuwa ni moja ya wahudhuriaji msibani hapo

wananchi wa jiji la Dar er salam walifurika nyumbani kwa Kanumba kwa ajili ya kujua kinacho endelea msibani hapo

Hapa ndipo palipokuwa nyumbani kwa kanumba ambapo mauti yalimkuta akiwa katika nyumba hii

mke wa waziri mkuu akisaini kitabu cha rambirambi na pia kuwafariji wale wote waliofikwa na msiba huu mzito kabisa.

Samweli 6 pia alikuwepo katika msiba huu mzito. na pia walikuwepo mamia ya wakazi na maeneo ya jirani na dar es salam

 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Taarifa zilizopo mtaani kwa sasa ni kuhusu kifo cha msanii wa maigizo na filamu nchini tanzania namzungumzia Steven kanumba amabye katika hali ya kushtua sana nilipata taarifa za kifo chake kutoka kwa rafiki yangu wa karibu mida ya saa kumi alfajiri ya leo na kwakweli nilipata mshtuko mkubwa na ilinikumbusha sana kifo cha marehemu kaka yangu amabye nae alifariki mida ambayo kanumba alifariki na ilikuwa ni ghafra sana kama ambavyo kimetokea kifo cha kanumba. Chanzo cha kifo cha kanumba mpaka sasa bado ni kitendawili ambacho wengi hatukufahamu ila kwa taarifa ambazo sio rasmi sana ki ugomvi wa mapenzi baina yake yeye na mpenzi wake Lulu taarifa hizo pia zinzfafanua kuwa Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU(Kwa sasa msanii wa kike Lulu pichani anashikiliwa na police kwa maelezo zaidi) 
kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.
pia inaaminika kuwa 
chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.

 haya ni mambo ya mwisho kuyandika kanumba katika face book na twitter hii ni kutoka millard ayo website.na baadhi ya maoni ya watu kupitia facebook

na hii ni post au habari yake ya mwisho katika blog yake ya kanumba the great. ambayo ameiandika jana april 6 2012.

HAPPY 5TH ANNIVERSARY TMH,SAMBAMBA NA UZINDUZI WA DUKA/OFISI & TRAINING CENTER

SEHEMU YA DUKA LA NGUO TOKA KWA DESIGNER MBALIMBALI.
TULIOSAPOTI MPAKA KITUO HIKI KUFIKIA HAPA KILIPO SOMA MAJINA HAPO JUU JINA LANGU LIPO HAPO,KUSEMA UKWELI INAPOKUJA MAMBO YA KUSAIDIA JAMII NAJITAIDI KUTOA NINACHOKUA NACHO MAANA HAPA HUKUMBUKA MANENO YA MWANDISHI ALBERT PINE..''"What we do for ourselves dies with us. What we do for others and the world remains and is immortal."
'' KANUMBA THE GREAT PIONEER MOTO WA VOLCANO'' NIKIWA KTK OFISI ZA TANZANIA MITINDO HOUSE.
Pia amecheza filamu nyingi na maigizo mengi katika kundi la kaole sanaa group na hizi ni filamu chache alizo cheza Steven Kanumba.
    JOHARI, DAR TO LAGOS, THA BIG DADDY, MOSES, SHE IS MY SISTER, BECAUSE OF YOU, DEVIL KINGDOM, THIS IT IS, MORE THAN PAIN,OFF SIDE,UNCLE JJ,DECEPTION, THE SHOCK, NK. 


 BAADHI YA WASANII NA WATU MAARUFU WAMIMINIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU WAKIWA NA MAJONZI MAKUBWA. picha na dj choka.
swahiba mkubwa wa Knumba Ray

baadi ya waigizaji na wasanii wafilamu wakiwa na majonzi

huzuni imetawal kwa kila mmoja najua hata wee imekugusa.

baadhi ya wasanii wa maigizo na filamu.


maoni ya wadau mbalimbali na watu maarufu yazidi kumiminika 
haya yalikuwa ya zitto kabwe.....mungu amekuchukua mapema sana. Umetuachia majonzi makubwa mno. Tangulia. Tuwekee nafasi huko. Kungekuwa na rufaa.......... 
haya yalikuwa ya salama jabir......Rest In Peace Steven...M/Mungu Alikupenda Zaidi. Rest In Peace My Brother 
haya yakikuwa ya Happnes Magesse......Rest in Peace my friend...you create jobs ,you believed on our own...and you took them as ur own and give them opportunities to believe on themselves and be who they wanna be and take acting as their career....Where do they go now.....Kanumba!!!? Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi...Pigo la taifa jamani..Poleni Kaole poleni Tanzania...!

haya yalikuwa ya roma mkatoliki.......
Dakika...chache baada ya show yangu ya musoma!! Napata taarifa za huu msiba wa THE GREAT K.A.N.U.M.B.A....sikuamini mpaka nilipopiga simu kwa mmoja wa mtu wake wa karibu na kunijibu huku analia kuwa bro hatunaye kweli na ndo' wao wanatoka muhimbili!!....ni msiba mzito na umewagusa wengi nikiwemo!! Pole sana kaole...pole game 1st quality...pole kwa mpinzani wake mkubwa Ray....pole kwa ben swahiba wake sana....dah pole kubwa kwa pacho mwamba!familia yake Na bongo movie wote...pamoja na watanzania wote!! TUTAKUKUMBUKA KWA MENGI KAKA STEVE.....Tumuombee ndugu ye2 apumzike pema peponi!!na asamehewe dhambi zake!! Oooh kaka umetuacha ukiwa angali mdogo...inauma sana!!
haya yalikuwa ya Solo Thang..........R.I.P STEVEN KANUMBA,,,Mungu amekupenda zaid,,Pole kwa familia na ndugu wa karibu na wapaenzi wa bongo movie kwa ujumla,,,gone too soon Hommie!

haya yalikuwa ua irene Uwoya ..........Kwaheri rafiki wangu wa karibu, kwaheri mwalimu wangu wa filamu.. na hizi zilikuwa ni shutma zake kwa Lulu..SIKU YA JUMATATU NILIANGALIA KIPINDI CHA MIKASI CHA SALAMA NDANI CHANEL 5 AMBAKO LULUA LIKUWA MGENI KATIKA KIPINDI IKO NAKUMBUKA KUNA SHWALIA ALIULIZWA KAMA ANA MPENZI AKAJIBU YEYE BADO NI MTOTO HANA MPENZI LAKINI MUNGU AONGOPEWI HATA SIKU MOJA NI SIKU TANO TU ZIMEPITA SASA MTOTO HUYU ANAUMBUKA KWA KUHUSISHWA NA KIFO CHA STEVEN KANUMBA AMBAYE JIPU LIMEPASUKA KUWA NDIE ALIKUWA MPENZI WAKE JAPO ILIKUWA SIRI SASA YAMEFICHUKA HAKIKA IMENIUMA SANA NAOMBA DOLA IFUATE MKONDO WAKE HUYU MTOTO AADABISHWE.
.

   Alale pema peponi Steven Kanumba bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe milele na hii ni safari ya wote ametangulia sisi tupo nyuma yako.. amen

 imeandikwa na Steven mruma na kupitia vyombo vingine vya habari. na taarifa zaidi zitakujia na matukio mbambali mbali kusu kifo cha kipenzi cha watu wajina wangu Steven Kanumba. 
toa maoni yako....


Post a Comment

Google+ Badge