Translate this blog in your favourable language

Tuesday, April 10, 2012

NA HII NDIO ILIKUWA SAFARI YA MWISHO YA STEVEN KANUMBA.

katika hali ambayo mimi niliitegemea kabisa ni mkusanyiko usio na mfano katika safari nzima ya kumsindikiza Steven Kanumba katika safari yake hii ya mwisho ambyo iliambatana na msongamano mkubwa watu hali iliyohatarisha pia maisha ya watu lakini hakuna madhara hasa ya watu kufa ila wengi walizimia kutokana na hali mbalimbali ikiwemo majonzi na msongamano na kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mooa amesema hakuna aliyeripotiwa kufa kutokana na mkusanyiko huo

na yafuatayo ni matukio katika picha kuhussiana na safari hiyo tangu leaders mpaka makaburuni kinondoni makaburini na baadhi ya picha ni kutoka katika mitandao tofauti.

Hapa wakijiandaa kutumbukiza mwili wa kanumba kaburini katika makaburi ya kinondoni

Swahiba wa karibu wa Kanumba[ Ray] alukuwa akishuhudia kwa karibu hatima ya rafiki yake kipenzi


hapa jeneza likiandaliwa kuwekwa kaburini

baadhi ya watu wakitoa heshima zao za mwisho katika mazishi ya kanumba

kulingana na idadi kubwa ya watu ulinzi uliimarishwa kila pande kuhakikisha kuwa watu wanakuwa na amani mda wote

baadhi ya wasanii waliowahi kuogiza na kanumba wakiwasili eneo la tukio kwa ajili ya mazishi

hiki ndicho chumba ambaco ndani yake amelala kanumba the greate

watu mashuhuri wakitoa heshima zao za mwisho kama ambavyo inaonekana

mama wa kanumba akiwapungua mkono walihudhuria katika mazishi ya mwanae kanumba

jeneza la kanumba likiwasili viwanja vya leaders mapema leo likiwa limebebwa na wasanii wenzake

Hemedi na Mlela wakiwasili viwanja vya leaders

hali haikuwa hali leaders wengi walizimia na ililazimu kazi ya ziada kwa wahudumu wa msalaba mwekundu

mama Salma kikwete akitoa heshima zake za mwisho viwanja vya leaders leo

kamanda Kova akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa kanumba mapema leo

jeneza la kanumba likiwasili leviwanja vya leaders mapema asubui leo likiwa limebebwana wsanii wenzake akiwemo Issa musa Cloud na wengine.
                      Leo ndio ilikuwa siku ya mwisho ya kumsindikiza Kanumba katika makao yake ya milele na hakika daima atakumbukwa kwa mengi na pengo lake wakuliziba simuoni ila cha msingi ni kuendeleza yale mema yote aliyoyafanya katika ulimwengu huu.
                  MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA STEVEN KANUMBA
                                                                             AMEN. 
Post a Comment

Google+ Badge