Translate this blog in your favourable language

My pager view

Friday, December 31, 2010

JE MWAKA MPYA UNAMAANISHA NINI KWAKO JE UNAMALENGO GANI? JE ULITELEZA NA UTAREKEBISHA WAPI?


TAMBUA MWAKA MPYA NA NINI CHAKUFANYA KATIKA MWAKA HUU WA MABADILIKO 2011
Mwaka mpya ni siku ya kwanza ya mwaka na mara nyingi ni sherehe na nafasi ya watu kutakiana heri na baraka za mwaka mpya.

Katika tamaduni mbalimbali nafasi hii ni sikukuu moja au zaidi pasipo na kazi za kawaida.
Tarehe ya mwaka mpya inategemea kalenda yake:
katika sehemu kubwa ya dunia inayotumia kalenda ya Gregori ni 1 Januari
Uajemi, Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Azerbaijan, Turkmenistan na Kashmir husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiajemi kwenye sikukuu ya Nouruz ambayo ni sikusare ya bubujiko inayotokea kati ya tarehe 20 - 21 Machi kwenye kalenda ya Gregori lakini kwao mwezi na mwaka mpya unaanza
Wachina na Wavietnam husheherekea mwaka mpya wakati wa mwezi mwandamu wa pili baada ya solistasi ya majira baridi na hii inacheza kati ya 21 Januari na 21 Februari.
Nchi ya Israeli na Wayahudi husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya kiyahudi kwa jina la rosh hashana ambayo ni siku inayotokea kati ya Septemba na nusu ya kwanza ya Oktoba.
Waislamu na nchi ya Saudia huwa na mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiislamu. Kalenda hii inafuata mwezi tu kwa hiyo sikuu zake huzunguka katika mwaka wa jua.
Sikukuu ya Diwali inasheherekewa na jumuiya kadhaa pia kama mwaka mpya.
Nje ya mahesabu haya kuna kalenda nyingine zisizoanzisha mwaka kwa sherehe. Mifano ni:
mwaka wa shule
mwaka wa biashara ambako hesabu mpya inaanzishwa
mwaka wa kanisa ambayo katika sehemu kubwa ya Ukristo unaanza kwenye jumapili ya Adventi (majilio) ya kwanza. kwa ufupi unaweza ukatambua kuwa mwaka mpya unamaana gani kwako na kwa ujumla wake lazima utambue kila unachopaswa kufanya kila mwaka na hayo ndio malengo yanayo leta mafannikio katika maisha kubali changamoto songa mbele
 NACHUKUA NAFASI HII KUKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA NA MUNGU AUONGOZE MWAKA WAKO UWE NA MAFANIKIO YALIOTUKUKA MBELE YA MUUMBA WAKO ....
 PIGANIA MAISHA YAKO AMINI DAIMA UTASHINDA...... NA USHINDI NI LAZIMA...