Translate this blog in your favourable language

My pager view

Saturday, December 11, 2010

UMUHIMU WA MAJI KATIKA MIILI YETU LAKINI BADO TUNALALAMIKA MAGONJWA MENGI WAKATI DAWA TUNAYO NA NI RAHISI [MAJI]

Maji ni hitajio la dharura kwa afya zetu, kwani asilimia 60 ya uzito wako ni maji na kila mfumo wa mwili wako hutegemea maji ili kufanya kazi zake. Ukosefu wa maji mwilini humfanya mtu akaukiwe na maji au dehydration, hali ambayo hutokea pale mtu asipokuwa na maji ya kutosha mwilini ya kuuwezesha mwili wake kufanya kazi zake za kawaida. Hata katika upungufu mdogo wa maji mwilini, wakati ambapo asilimia 1 hadi 2 ya uzito wa mwili inapopungua, huweza kumfanya mtu akose nguvu na ajisike amechoka. Miongoni mwa dalili za upungufu wa maji mwilini ni: • Kukihi kiu sana • Uchovu • Kichwa kuuma • Mdomo kukauka • Kukosa mkojo au kiasi cha mkojo kuwa kidogo. • Udhaifu wa misuli • Kuhisi kizunguzunguNi muhimu kujua kwamba mwili hupoteza maji kila siku kwa kutokwa na jasho, iwe jasho hilo umelihisi au haukulihisi, kutoa pumzi nje (exhaling), kukojoa na harakati ya tumbo. (bowel movement).
Ili mwili wako uweze kufanya kazi vizuri unahitajia kurudisha maji hayo mwilini kwa kunywa vinywaji mbalimbali na vyakula vyenye maji.
Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa mwanadamu anahitajia kunywa vikombe 8 vya maji kwa siku, ili kufidia maji yanayopotae mwilini. Hata hivyo wengine wanashauri kwamba, wanaume wanywe vikombe 13 vya maji kwa siku na wanawake vikombe 8 vya maji, na hiyo ni kutokana na tofauti ya miili yao. Tunashauriwa kuwa badala ya kunywa maji kiholela tunywe kwa mpangilio maalum kwa siku, ili kusaidia vyema katika kazi za mwili. * Tunashauriwa kunywa vikombe viwili vya maji asubuhi pindi tunapoamka, kwani husaidia kuamsha viungo vya ndani ya mwili.* Tunashauri tunywe kikombe kikoja cha maji dakika 30 kabla ya mlo, kwani husaidia kupata choo vizuri.* Tunashuariwa tunywe kikombe kimoja cha maji kabla ya kwenda kuoga, husaisia kupunguza shikizo la damu.* Na tunashauriwa kunywa kikombe kimoja cha maji kabla ya kulala kwani kufanya hivyo huzuia shinikizo la moyo.