Translate this blog in your favourable language

Tuesday, December 14, 2010

HUYU NDIE HAYATI REMMY ONGALA NGULI WA MUZIKI AFRIKA NA DUNIA [ALIPOTOKA NA ALIPOFIKIA TAMATI]
Remmy Ongala (1947 - Desemba 13 2010) alikuwa mwanamuziki nchini Tanzania mwenye asili ya Zaire. Alizaliwa na jina la kiraia la Ramadhani Mtoro Ongala katika jimbo la Kivu la Kongo ya Kibelgiji.
Remmy Ongala pamoja na bendi yake ya Super Matimila, ni mashuhuri sana nchini Tanzania, na wamepiga muziki mara nyingi katika nchi za Ulaya na Marekani. Remmy Ongala kwa asili anatoka Zaire. Akiwa na umri wa miaka tisa mama yake alifariki, hivyo ikimbidi achukue jukumu la kutunza wadogo zake.
Akiwa na umri wa miaka 17, alikuwa muimbaji na mpiga ngoma katika bendi ya vijana ya Bantu Success. Hii haikuwa na maana kwa familia yake, hivyo Remmy ilimbidi atoke katika bendi. Miaka miwili baadaye, alijishughulisha tena na muziki. Alijiunga na vikundi mbalimbali vya bendi za muziki akiwa mpiga gitaa, baadhi yake zilikuwa Micky Jazz ya Zaire na Grand Mike Jazz ya huko Uganda. Mwaka 1978 alihamia Tanzania na kujiunga na bendi ya mjomba wake Ochestre Makassy ya jijini Dar es Salaam.
Mwaka 1981 alijiunga na bendi ya Matimila, ikiwa na wanamuziki 18 na ikimilikiwa na mfanya biashara mmoja. Baadaye alianzisha bendi yake ya Super Matimila na kuendeleza mtindo wa kutumia magitaa 3, besi, ngoma na tarumbeta aina ya saksafoni. Remmy Ongala alipiga muziki wake kwa mtindo wa Soukous, katika maumbile mapya kabisa kwa kutumia asili na jadi ya kitanzania. Akiimba kwa kiswahili, ushairi wake mzuri una tunzi zinazohusu siasa na pia maisha ya mtu wa kawaida. Kwa ajili ya uimbaji na utunzi wake wa kuliwaza, Remmy anaitwa “Dokta” na ni mtu anayejulikana sana katika sehemu za Sinza ambazo ni jirani na anakoishi yeye na mkewe mwingereza na watoto wao 5 na kasuku mmoja, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

WASIFU WAKE KWA UJUMLA
Jina la kuzaliwa Ramadhani Mtoro Ongala
Amezaliwa 1947
Asili yake Mzaire, Mtanzania
Amekufa 2010
Kazi yake Mwimbaji
Ala Sauti, Gitaa
Miaka ya kazi mn. 1965 -
Ameshirikiana na Virunga, Diblo Dibala, Orchestra Super Mazembe, Orchestra Makassy
japo kwa ufupi ila kamwe hatasahaulika hayati remmy ongala lakini pia ikumbukwe kuwa remmy aliwahi kuokoka na alitumikia kipindi chake cha kuokoka kwa kuhubiri injili na kuimba nyimbo nyingi za injili mpaka aliporipotiwa kufariki dunia tar 13/12/2010 mungu ailaze roho yake mahali pema pepeni
amina..
na steven mruma kwa msaada wa vyombo vingine vya habari duniani...
Post a Comment

Google+ Badge