Translate this blog in your favourable language

Monday, November 8, 2010

MAKALA MAALUM YA UCHAGUZI MKUU ULIOFANYIKA 31/10/20101 TANZANIA NA CHANGAMOTO MPYA..

uchaguzi tangu kampeni hadi kuapishwa kwa rais dk. jakaya m. kikwete..............
HAYAWI hayawi, sasa yamekuwa, Uchaguzi Mkuu wa 2010 umefanyika na viongozi wamepatikana. Hii ni baada ya kampeni za takribani siku 70 za mchana na usiku, wengine wakiziita za nyumba kwa nyumba, kupasua anga na mwisho wake kufanyika kwa uchaguzi uliosababisha kupatikana kwa Rais katika uchaguzi wa nne kuvishirikisha vyama vingi vya siasa,
Mengi yamesemwa, kadhalika mengi yametokea, Watanzania hawakubadilishwa na kampeni, zilizofuatiwa na uchaguzi na baadaye matokeo. Tanzania imeendelea kuwa moja na Watanzania wameendelea kuwa walewale. Lakini je, nini haswa kimejiri kufuatia uchaguzi huu wa nne uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu?

Mwamko wa wananchi

Jambo muhimu ambalo Watanzania wameshuhudia katika uchaguzi huu wanne mwamko mkubwa wa wananchi. Wengi wamejitokeza katika mchakato mzima la kampeni za wagombea mbalimbali na hatimaye kupiga kura kwa wale walioona wamewaridhisha na wanafaa kuongoza.
Lakini wananchi pia wameonyesha utulivu wa hali ya juu katika zoezi zima la kampeni na hatimaye uchaguzi. Licha ya tofauti za kiitikadi, hakukuonekana kuwa na uhasama mkubwa baina yao zaidi ya kupingana kwa hoja.
Kutokana na mwamko huo wa wananchi, utulivu uliokuwepo uchaguzi umeonekana kufanyika katika hali ya amani na utulivu kulinganisha na uchaguzi uliotangulia, hali inayodhirisha ukomavu wa kisiasa.
Mwitikio wa wananchi

Kwa ujumla, kama ilivyokuwa katika kujiandikisha kupiga kura, wananchi HAWAJAJITOKEZA kwa wingi. Idadi ya waliojitokeza kupiga kura nayo imekuwa ni ndogo kulinganisha na ile ya chaguzi zilizopita.

Idadi iliyoonekana kuwa kubwa ni ile ya vijana. Hamasa kwao imekuwa kubwa na wachunguzi wa mambo wanasema wingi huo unatokana na shauku ya vijana wengi wenye umri mdogo ambao wengi wa vijana hao wanapiga kura kwa mara ya kwanza.
Ukiachilia mbali idadi kubwa ya vijana wanawake nao hawakuwa nyuma, katika vituo vingi, wanawake wengi wa rika mbalimbali walijitokeza katika vituo kupiga kura, kulinganisha na wanaume hususani watu wa umri wa katikati na wale wa makamo.

Kukua kwa demokrasia

Mchakato mzima umemalizika huku wananchi wakishuhudia mabadiliko makubwa ya kukomaa kwa demokrasia nchini. Hali ya ukomavu wa kisiasa na kukua huko kumeonekana wazi tangu wakati wa kampeni ambapo wananchi na wagombea walionekana kuwa wawazi kuzungumza hisia zao.

Tatizo jingine lilikuja baada ya matokeo ya baadhi ya maeneo mengi kuchelewa kutolewa na baadhi ya wananchi walonekana kutopenda kilicho tokea na hili lilizua tafrani kama vile mwanza na kazalika,…

Changamoto kubwa sana ndani ya matokeo yaliyotoka ni upinzani kuvunja record yake kwa kupata viti vingi zaidi bungeni kuliko kipindi kingine chochote kile na hili linazibitisha kua mwaka huu mjengono hapatoshi katika vyombo vya habari nilinukuu kauli ya msanii mr. sugu alieingia bungeni kupitia chadema kua atakua mtulivu kuliko waivyo mzoea wanachi wengi na hili linanipa shauku ya kufatilia bunge la mwaka huu

Ushingi kama wengi mnavyojua ulienda kwa jakaya kikwete na aliapishwa jumamosi lakini slaa alionekana kutoridhika kabisa na matokeo hayo

KILICHONISHANGAZA 58% YA WALIOJIANDIKISHA HAWAKUPIGA KURA NA HII IMENIPA TAHARUKI KUBWA KWAMBA MAAMUZI YA WATANZANIA YANAAMULIWA NA WATU MILIONI 8 TU????? KATI YA WATU MILIONI 20 WALIOJIANDIKISHA  HILI NI TATIZO KUBWA SANA TUME IFANYIE KAZI MANENEO YA IBRAHIM LIPUMBA SIKU YA KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA URAIS HALI HII INATISHA SANA

MWISHO NAWAPONGEZA WALE WALIOJITOKEZA KU[IGA KURA BILA KUWASAHAU WALIOENDELEZA AMANI KATIKLA KIPINDI CHOTE CHA UCHAGUZI

WABILAH TUFIQ,….

NA STEVE MRUMA.., TANGA
Post a Comment

Google+ Badge